Mwanafunzi Aliyefunika Hisabati Darasa la Saba

Mwanafunzi bora wa somo la Hisabati katika mitihani ya taifa ya darasa la saba iliyofanyika nchini Septemba mwaka huu, Rachel Kiunsi (13), ameeleza siri ya mafanikio yake kuwa ni kujituma katika masomo na kuwaheshimu walimu.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana kutoka mkoani Singida, Rachel ambaye alikuwa anasoma shule ya msingi Kimara 'B', jijini Dar es Salaam, alisema alikuwa na bidii ya kujituma katika masomo yake hasa katika la hisabati na   ya Sayansi na kwamba alikuwa anashindwa kupata usingizi bila kujisomea usiku.

Akizungumzia jinsi alivyopokea taarifa za matokeo yake, Rachel alisema ni kwa furaha na alikuwa akitengemea kufaulu, lakini siyo kwa mafanikio kama hayo aliyoyapata.  
“Nanamshukuru sana Mungu  kwani nilikuwa namwomba atende maajabu katika matokeo yangu... nilikuwa nasali kila nikifanya mtihani na kumaliza,” alisema Rachel, ambaye alikuwa akiishi na bibi yake Kimara.

Aliwashukuru walimu wake wa masomo yote kwa juhudi za kuwafundisha vizuri wanafunzi wote katika shule hiyo kwani walikuwa wakiingia darasani kwa muda wa ziada na kutoka saa 11 jioni.

“Mimi nawashauri wanafunzi wenzangu tuliomaliza wote na kufaulu kuwa tuongeze bidii katika masomo yetu ya Sekondari kwani bila juhudi hatutaweza kufaulu kama tulivyofaulu sasa,” alisema. 

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad