THT jana imemuaga rasmi Amini ambaye miongoni mwa mastar wanaotokea kwenye jumba hilo la vipaji Tanzania baada ya kuishi ndani yake kwa zaidi ya miaka 9 mpaka sasa.
Amini ambaye anakua msanii wa pili kutoka kwenye uongozi wa THT baada ya Linah ambaye aliagwa Mwezi July mwaka huu anasema ameishukuru sana THT kwa muda wote aliokuwa nayo kuanzia kama mwanafunzi hadi baadae kuwa mwanamuziki kamili.
Baada ya kukamilika kwa shughuli ya kutoa vyeti kwa walimu na uongozi wa THT akiwemo Mkurugenzi Ruge Mutahaba,Amini pia aliwapa nafasi waandishi na waalikwa kushuhudia kipande cha video ya wimbo wake mpya uitwao Mbeleko.