Stori: Hamida hassan na Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula (pichani) maarufu kama Johari, hivi karibuni alidaiwa kuonekana akiingia nyumbani kwa mganga wa kienyeji (jina linahifadhiwa) katika Kijiji cha Kibeta, mjini Bukoba mkoani Kagera.
Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa Johari akiwa katika bodaboda, aliingia kwa mganga huyo wa kike anayefahamika sana eneo hilo.
“Sijui nilikuwa namfananisha? Nimemuona msanii wenu hapa Kibeta akiingia kwa mganga ila nimeshindwa kumpiga picha maana kasimu kangu ni ka’ tochi, labda kaja kuweka mambo yake sawa,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa habari hizi, mwandishi wetu fasta alibonyeza namba za Johari katika simu yake ambaye alikiri kuwepo Bukoba kwa siku mbili kwa shughuli zake.
“Jamani siyo kila kitu muandike, mmejuaje mimi nilienda Bukoba, naomba hii isiwe habari tafadhali si ulimwengu mzima ujue mimi nimefanya nini,” alisema Johari, mmoja wa waigizaji nyota na mkurugenzi mwenza wa RJ Company.
Katika kujitetea zaidi, Johari alisema alikwenda Bukoba kwa mama yake mkubwa, (jina linahifadhiwa) ambaye hakujua kama anajishughulisha na mambo ya uganga kwani hakuwahi kusikia.
“Sikupenda hii habari kabisa, lakini kiukweli nilienda kumuona mama yangu mkubwa nikiwa na ndugu zangu wengine, kwani alikuwa akiumwa, sikukaa sana, nilikaa siku mbili tu na kugeuza kwani nilikuwa nikitokea Shinyanga kwenye msiba kama ulisikia nilifiwa,” alisema na kuongeza kuwa hajawahi kupanda pikipiki kwani magari yapo tena kwa bei rahisi.
Mwigizaji Johari Adaiwa Kunaswa Kwa Mganga wa Kienyeji Akifanya Mambo
0
November 28, 2014
Tags