Mwigulu Nchemba Acharuka Asema Walio iba Fedha za Escrow Wakamatwe na Kufilisiwa Mali zao

Mwigulu Nchemba alitoa msimamo mkali kuhusu sakata hilo la escrow na kwamba ametaka hatua zichukuliwe kwa wahusika wote.

Katika kikao hicho inaelezwa kwamba Nchemba alionyesha msimamo wake waziwazi kuwa sakata hilo ni hujuma  na kwamba haiwezekani walioiba fedha hizo wakaachiwa tu hivihivi.

Ndani ya kikao hicho imeelezwa kuwa Mwigulu alijitokeza na kusema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameshamaliza utata hivyo, mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe.

Alisema haiwezekani watu wakawajibika tu kwa kujiuzulu kwa kuwa huko ni kutoa tu likizo mtu akale mabilioni yake, hivyo wachukuliwe hatua ipasavyo na kufilisiwa.

“CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote na wahusika wote wakamatwe,” alisema Mwigulu.

Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu taifa wakamatwe na akaunti zao zikamatwe, zifilisiwe na fedha zirudishwe kwa wananchi.

Pia aliagiza mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye anatuhumiwa kuchota Sh1.6 bilioni za akaunti hiyo afukuzwe kazi, akamatwe na akaunti zake za fedha zifilisiwe ili fedha irudi serikalini.

Habari za uhakika kutoka kikao hicho zinaeleza kuwa Mwigulu aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri Mkuu na kusema kuwa kujiuzulu siyo adhabu stahiki kwa wizi mkubwa kama huo.

Mwigulu alisema: “Tazama wanafunzi, watoto wa maskini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna, maskini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai fedha zao, wazabuni wanauziwa nyumba zao na benki huku wakiidai Serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzulu? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia maskini?”

Kwa mtumishi wa TRA aliyekula fedha za IPTL zaidi ya 1.6 bilioni Mwigulu akatoa agizo:

Nimemwagiza Kamishna wa Kodi amfukuze kazi yule mtumishi wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe na wahusika wakamatwe.

Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga maskini na kuwapa likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini,” Mwigulu alisisitiza.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad