Naombeni Ushauri Wenu, Mpenzi Wangu Amekutwa na Maambukizi ya Ukimwi

Jamani nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mdada mmoja hivi takribani ni miaka 3 sasa.

Katika mahusiano yetu tumekuwa tukipendana sana na hatma ya yote lengo letu lilikuwa ni kuishi wawili kama mume na mke.

Huyu mpenzi wangu tumekuwa tukiishi mbali mbali kutokana na wote wawili kuwa na majukumu tofauti ya kiutumishi.
Hapo mwanzo nilipoanza nae tulipima afya zetu yaani hatukuwa na maambukizi ya vvu.

Kiukweli tokea hapo tulijihusisha na mapenzi kwa uaminifu kila upande. Nimekuwa nikimuamini sana na yeye pia kuniamini. Mimi mwaka huu nilikuwa nimepanga tufunge ndoa mwezi wa 12. Mimi naishi mwanza kikazi ila yeye anaishi dodoma.

Tokea mwanzo wa mahusiano yetu sijawahi kutumia kinga ninapokutana na yeye na nimekaa naye kwangu mara nyingi sana pindi anapokuwa na likizo.

Mwezi uliopita amekuja kwangu nikawa nimekaa nae kama wiki mbili hivi akawa amepata homa tu ya kawaida.

Ikabidi nimpeleke hospitali kupata matibabu,tulivyoenda hospitali nikamshauri ebu leo tucheki bas afya zetu? Kwani ni muda sasa hatujacheck vvu.

Alikubali tukawa tumeenda kupima,majibu yaliyotoka ni kwamba yeye ana maambukizi ya vvu na kwa upande wangu sijaonekana na maambukizi.

Kiukweli hiki kitu kimeniumiza sana na hapa nilipo sijajua hatma ya maisha yangu,na daktari alichoniambia ni kwamba mimi damu yangu sio rahisi kupokea maambukizi ya vvu kutokana na group langu la damu na lake.

Hivyo amenishauri niendelee kupima kila baada ya miezi mitatu ili kuwa na uhakika zaidi.

Kitu kinachoniumiza na kunisumbua kichwa zaidi ni kwamba huyu mchumba wangu analia sana na anasema kutengana na mimi ni bora yeye afe tu kuliko kukaa mbali na mimi.

Na kingine ni kwamba,anadai kutokana na upendo wangu juu yake anataka anizalie mtoto ili aniachie zawadi hata yeye akifa.

Kiukweli hapa nilipo sijitambui afya yangu na kushiriki tena tendo na yeye naogopa.

NIFANYAJE Ili kumfurahisha? nikubali kuzaa nae? Nifanyaje 

Top Post Ad

Below Post Ad