Rapa mkali kabisa kutoka Uganda, Navio ambaye kwa sasa yupo hapa nchini Tanzania kwa shughuli za kimuziki, amewataja wasanii Shaa, Diamond, Joh Makini, Izzo Business, Vanessa Mdee na AY kama wasanii kutoka hapa Bongo ambao anawakubali zaidi.
Navio ameiambia eNewz kuwa, kazi za wasanii hawa pamoja na moyo wao katika kazi ni kati ya vitu vinavyomfanya kuwaelewa zaidi pamoja na kufurahia kazi zao.
Rapa huyo pia ameweka wazi uwezekano wa kufanya kolabo na wasanii kutoka hapa Tanzania, akiwa tayari katika maongezi ya awali na msanii Izzo Business.