“WANANIITA mshamba wa Kimanyema ila poa tu!”Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema baadhi ya mashabiki wake wanamuita mshamba wa Kimanyema, lakini hilo halimsumbui na wala halimpi presha.
Nyota huyo anayetamba na wimbo ‘Ndagushima’, amesema hawezi kuacha kufurahia kupiga picha nyingi iwezekanavyo anavyosafiri nje ya nchi kwani ni kumbukumbu kwake na pia ni kitu alichokiota kwa muda mrefu.
“Eti wanasema mshamba wa Kimanyema kapata vihela vyake eti kaenda shopingi, nifanyaje sasa na ni kitu ninachokipenda, sitaacha kutupia picha nikiwa nje au ndani ya nchi kwa kuwa ni kitu ninachokipenda na nadhani wengi wanapenda kwani ni sehemu ya kufurahia maisha,” alisema Ommy Dimpoz.
Msanii huyo amekuwa katika ziara ya wiki mbili sasa katika nchi mbalimbali ambapo kesho Jumamosi, atatumbuiza katika Ukumbi wa La Bodega huko Ufaransa baada ya shoo iliyofanyika wiki iliyopita katika mji wa Rotterdam, Uholanzi.
Achana nao hao wanakuonea WIVU! Usikwazike mwanangu ukashindwa kuendelea na mambo yako. FANYA YAKO! ni wivu tu unawasumbua. UKO JUU!
ReplyDeleteWEE MANYEMA WALA WASIKULAZE PRESSURE JUU! SASA KAMA NI WA KIGOMA SHIDA IKO WAPI KWANI KIGOMA SIO TANZANIA? ACHANA NAO KULA MZIGO MPAKA KIJULIKANE NAONA KWA SABABU WAO HAWAWEZI KUJA MAJUAA BASI IMEKUWA NONGWA, KAZA BOOT. KIGOMA OYEE !!!!! UJIJI OYEEE, KASULU OYEEE, KIBONDO OYEEE!!!! BONGO FLAVA WAKUBALI WASIKUBALI NI VIAJANA WA KIGOMA NDIO WAMESHIKA USUKANI...LEKA DUKITIKE
Delete