Rais Jakaya Kikwete Afanyiwa Upasuaji Nchini Marekani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.
Hali ya MheshimiwaRais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wao wakiumwa wanakwenda Marekani, sisi tukiumwa tunachemsha mizizi maana hospitali za serikali dawa hakuna sababu ya deni la MSD............TZ ni sheeeeeeeedar!

    ReplyDelete
  2. Mungu awabariki wakuu siku isiyonajina itawadia olewenu

    ReplyDelete
  3. Naomba mnitafusirie Uo Ugonjwa kwa kingereza ni rahisi kujua,maana viswahili vya bongo ni vigumu,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad