Ray: Chuchu Ndio Kila Kitu Kwangu, Johari na Mainda Tupa Kule

Stori: Musa Mateja
LEGENDARY kwenye anga la sanaa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans ndiye kila kitu na kilichobaki ni ndoa tu.

Akizungumza na paparazi wetu, Ray alisema licha ya kupitia katika changamoto nyingi za mapenzi lakini kwa Chuchu amefika na haoni tabu kujinadi kwa mtu yeyote juu ya penzi lake hilo.

“Chuchu ndiye kila kitu kwangu, tunaendana kwa kila kitu hivyo nitakaowaudhi kwa kumpenda yeye, wanisamehe,” alisema Ray.Ray kabla ya kuwa na Chuchu, kwa nyakati tofauti alikuwa akitajwa kushea penzi la mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’ na Blandina Chagula ‘Johari’.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad