Katibu Mkuu wa ACT- Tanzania Samson Mwigamba amesimamishwa uongozi ndani ya chama hicho kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili,kuvunja katiba na ubadhirifu ndani ya chama hicho.
Taarifa kutoka kwa waasisi wa chama hicho ambao ni Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona zinasema mbali na Mwigamba pia chama hicho kimetoa karipio kali kwa viongozi waandamizi wa chama hicho Professor Kitila Mkumbo na Habib Mchange kwa tuhuma mbalimbali.
Ikumbukwe Samson Mwigamba,Prof Kitila Mkumbo na Zitto Kabwe walitimuliwa uongozi ndani ya CHADEMA mapema mwaka huu kwa tuhuma kama hizi na kusababisha kukimbilia chama cha ACT Tanzania.
Source:Mtanzania Jumatano
Updates zaidi....
Waasisi wa ACT Tanzania Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona waliwaambia waandishi wa habari jana kuwa waliwakaribisha Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba ndani ya chama hicho kwa nia njema kumbe ni wasaliti na walaghai wakubwa.
Alisema kwanza kina Mwigamba wanajivika uasisi wa ACT huku wakijua si kweli. Pia kina Mwigamba wanatuhumiwa kwenda ofisi ya Msajili kubadili nembo ya chama kinyume cha utaratibu. Pia wanatuhumiwa kusajili katiba nyingine kinyume na Katiba waliyoandaa waasisi na kupatia chama usajili.
Nyakarungu amesema tayari Waasisi halali wa ACT wameshamwandikia barua msajili wa vyama kumuelezea juu ya uasi unaofanywa na kina Mwigamba na Kitila