Sendeka Asema Tutauana Lakini Pinda Hajiuzulu Katu

SENDEKA asema tutauana lakini PINDA hajiuzulu katu. 
Kikao cha wabunge wa CCM kinachiendelea mchana huu kimekuwa moto mbali. Christopher Ole Sendeka mbunge wa Simanjiro amesema wako radhi kuchinjana bungeni lakini si Pinda kujiuzulu. "Ajiuzulu amekosa nini, ripoti zote hazimtaji popote kuhusika. Kama tatizo ni nia yake ya u Rais, kwani Pinda hana haki ya kugombea? Nasema niko radhi tuchinjane bungeni lakini si kuona mtu anasulubiwa kwa maslahi ya wabinafsi wachache wenye malengo yao ya kisiasa. Kwa hili nitasimama kidete. .."alisema Sendeka huku ukumbi wote ukiwa kimya
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad