SERIKALI ya Tanzania imeshtushwa na ripoti inayoelezea biashara haramu ya pembe za ndovu kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China.
Serikali hiyo imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa Kichina wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania ndio wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya pembe za ndovu.
Inadaiwa kwamba raia wa China walitumia ziara ya rais wao, Xi Jinping ya nchini Tanzania kusafirisha kimagendo maelfu ya kilo za pembe za ndovu.
Kulingana na shirika la utafiti wa mazingira, EIA, Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja kabla ya ziara ya rais huyo nchini mwaka jana na zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili zisitambuliwe.
Msemaji wa Serikali Assah Mwambene amemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar famau kwamba ripoti kama hiyo zinatatiza jitihada za serikali kukabiliana na uuzaji haramu wa pembe za ndovu.
CHANZO: BBCSWAHILI
Kama ni za uongo waishtaki BBC na Aljazeera walete uthibitisho!We have have leaders and civil servants and including large part of population which have targeted short term benefits.Ndio maana pesa za kujenga hospitali au huduma muhimu zinatumiwa kwa shughuli binafsi.Viongozi wanachukua nyumba za serikali na kuzipangisha.Ni mzunguko wa rushwa na ufisadi na kinachosikitisha ni kwamba wananchi wamekubali kuwa ndio mfumo wetu wa maisha au tumeumbwa tuwe hivyo.
ReplyDeleteMindiomaana naona wakifa tu itakuwa vizuri siwashakulasana wapungue wapishe wengine.mijitu miroho milafi mibinafsi wafe tu
ReplyDeleteWanakanusha nini? wakati ndio mambo yanayofanyika, wenyewe wanazani siri, kumbe hamna siri, urimwengu sasa unakoendea, ni teknologia zaidi, na kuna kuwa na ukweli na uwazi, ndio mambo mnayofanya haya , kwenye mataifa yenu, Viongozi wasiojielewa, shame on u. kuendekeza ufisadi na kutaka maisha ya kifahari kama kiongozi uku mnangamiza Taifa.
ReplyDeleteMnamaaliza tembo wetu mnatuhonga uprofesa wa kichina?
ReplyDelete