Nimrod Mkono amekoswakoswa kuuawa nchini Uingereza alikokuwa amekwenda kikazi. Aliwekewa sumu ambayo ilipaswa iharibu kabisa figo zake ndani ya saa 72. Uongozi wa bunge umethibitisha na ripoti ya madaktari wa London inaonesha hivyo. Mkono mwenyewe anasema alionywa kuwa usalama wake uko mashakani na akatakiwa asifikie katika hoteli ambayo ujumbe wa viongozi wa Tanzania utafikia. Mkono anasema alipofika London aliamua kwenda katika nyumba yake binafsi, lakini baadaye alianza kutoka jasho, kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu kwa saa 6. Ikumbukwe kuwa Mkono na kampuni yake ya Mkono & Advocates ndiyo iliyokuwa inatetea upande wa TANESCO na Serikali katika kesi dhidi ya IPTL. Inasemekana Mkono anatafutwa kuuawa kwa sababu inaonekana ana taarifa nyingi mno kuhusu sakata la IPTL na ESCROW, na serikali inamtuhumu kuwa yeye ndiye aliyevujisha nyaraka zote hadi umma wa watanzania kugundua kuwa zaidi ya bilioni 321 mali ya umma zimeibiwa katika sakata hilo.