Kama umepitwa na U Heard kwenye XXL ya leo nimekuwekea hapa, zimesikika taarifa kuhusu Kala Jeremiah na Ney wa Mitego.
Baada ya tetesi nyingi kuenea mtaani kuhusu wasanii wawili ambao walikuwa hawaongei karibu miezi mitano kisa kikidaiwa ni mambo ya nyimbo zao.
Mwezi wa sita msanii Kala Jeremiah aliachia nyimbo ya ‘Simu ya Mwisho’ alichomshirikisha Ney wa Mitego, haukupita muda mrefu Ney akaaichia Mr. Ney ambapo ndani yake alimtaja Kala Jeremiah kuwa kapotea kwenye game na huo ukawa mwisho wa wasanii hao kuwasiliana kama ilivyokuwa zamani.
Wakali hawa wamekutana Ubungo kwenye studio ya mtengeneza Video, Pablo na maongezi yao yalikuwa poa, kama watu ambao hawana tofauti yoyote.
U Heard nimekuwekea hapa, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.