Ukweli Kuhusu Safari ya Jaji Mkuu Washington DC, Maafisa Wake na Francis Nyalali

Tumefanya uchunguzi hapa DSM na huko Washington DC kufuatilia hicho kinachoitwa semina ya majaji
iliyofanyika USA ambayo ilijaza na maafisa wakuu wa mahakama. uchunguzi wetu ulianzia ubalozi wa marekani 
hapa dsm eneo la Drive inn kupata ukweli juu ya semina ya majaji hao lakini ktk kitengo chao cha habari kwa
Bw. MOORE akatuambia hakuna kitu kama hicho kuhusu mualiko wowote unaousiana na semina ya majaji au wanasheria uliopita ubalozi huo.

Tukatoka hapo tukawasiliana na ubalozi wa Tanzania uliopo washington DC kupata maelezo yeyote kuhusiana na semina yeyote ya majaji inayoendelea huko ofisa wa ubalozi alisita kwanza lakini baadaye walituambia kuwa hawawezi kushea information kama hizo na sisi kwahiyo tuwasiliane na wausika. Tukaenda kwenye website ya mahakama kuu ya marekani kuona kama kuna tangazo lolote kuhusu semina hakuna kitu kama hicho tumekuta matukio mengine lakini hakuna issue ya semina. Tumewasiliana na wahusika akiwemo jaji mmojawapo kwy ule msafara simu zao zinaita hazipokelewi.

Conclusion yetu

Kulingana na uchunguzi wetu tumeitimisha kuwa jaji mkuu pamoja na maofisa wa mahakama walikwenda Washington DC kwa ajili ya kitu kimoja tu nacho ni kujadili suala zima la issue ya acount ya Escrow na mpaka hivi sasa hakuna ushahidi wowote kuhusiana na uwepo wa semina unless watoe picha zinazoonesha semina hiyo ambayo wahusika walidai walikwenda kuhudhuria na siyo kuonana na JK.

Swali kubwa ambalo inabidi watanzania tujiulize hivi ni kweli mahakama zetu ni huru ?? kwa mujibu wa uchunguzi wetu ni kuna muingiliano wa hali ya juu kati ya mahakama na executive kwa maana ya ikulu. Tunajiuliza kama jaji
mkuu na maofisa wa ngazi ya juu wa mahakama wanaweza kufunga safari kwenda kuonana na Rais kwa ajili kujaribu kupotosha nchi na kulinda mafisadi. Je Rais anapokuwa nyumbani ni mara ngapi jaji mkuu na maofisa wake wanakwenda ikulu kujadili na mkuu wa nchi kuhusu mienendo ya kesi mbali mbali na maswala ya ushahidi?? 

Hii inatupelekea kuamini kabisa maneno aliyoongea aliyekuwa jaji mkuu wa Tanzania Francis Nyalali kuwa mahakama za Tanzania si huru na zitakuwa huru tu endapo ikulu itakapoacha kuitisha na kuyajadili mafaili ya watuhumiwa ikulu.

Kitendo cha ofisa wa ngazi ya juu wa ikulu Bw.Ombeni Sefue cha kutoa tamko la kutojadiliwa issue ya ESCROW bungeni na kujigeuza messenger wa mahakama na kulitishia bunge kuwa linaingilia amri ya mahakama ni kosa la wazi na linathibitisha jinsi ikulu inapoingilia wazi uhuru siyo wa bunge bali na mahakama zetu.

By  Politiki/Jamii Forums
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad