Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kitendo alichofanya Freeman Mbowe cha kumsimanga wakati wa mikutano yake ya hadhara mkoani Kigoma kuwa amemsaidia sana ni cha kitoto.
Zitto amesema “nimeshangazwa na tabia ya Mbowe ya kunisimanga, tena kunisimanga nyumbani kwetu. Hata hivyo nimepuuza kwa maana kwa vyovyote vile aliongea bila kufikiri. Anasema nilitaka kusaliti chama, aseme kwa ushahidi maana kutamka tu hakuna maana hata kidogo.”
"Kiongozi mkubwa kama Mbowe anapaswa kujadili masuala ya Taifa na namna ya kutatua changamoto , sio kubaki kusema na kusimanga watu. Mbinu hiyo hailisaidii Taifa," Amesema Zitto.
“Mimi nina rekodi ya kujivunia … nimeibadilisha Kigoma na kusimamia ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege. Nimewezesha wakulima kuwa na hifadhiya jamii, bimna ya afya. Je, yeye kafanya nini Hai?” aliuliza Zitto.
Zitto aliendelea kusema "Nimeibua hoja za maana Bungeni zikiwemo ya kubadili sheria kwa manufaa ya nchi. Yeye kafanya nini Bungeni kwa manufaa ya nchi tangu aingie?Ametoa hoja gani binafsi? Ametunga sheria gani binafsi?