Jana katika bunge mwenyekiti wa PAC ZITTO KABWE alisimama bungeni na kuongea kwa fahari kuwa alihudhuria kikao cha UKAWA usiku uliopita. Kwa nafasi ya Zitto kama mwenyekiti wa kamati ambayo hoja yake iko mezani inajadiliwa, halikuwa jambo la sawa kuhudhuria kikao cha UKAWA na kusuluhishana, hasa wakati huu.
Zitto angebaki kuonesha neutrality ya ufuasi wa vyama, kwani katika kupitisha mapendekezo ya kamati yake anahitaji uungwaji mkono wa wabunge wa vyama vyote vikiwemo visivyounda UKAWA.
Zitto hakupaswa kukubali kutafuta suluhu na UKAWA wakati huu ambapo kamati yake imepewa dhamana kubwa ya kulivusha taifa katika sakata hili bila ya upendeleo wala uonevu. Kukubali wito wa suluhu na UKAWA ni sawa na matumizi ya nafasi yake kwa maslahi binafsi ya kujijenga kisiasa. Hii ndiyo tafsiri ya rushwa, abuse of public office for the private gain.
Hata kama hakujua haya, hakukumbuka busara na akahudhuria kikao cha UKAWA , halikuwa jambo sahihi kulisema mbele ya bunge tukufu. Kufanya vile kuliashiria kuwa Zitto amechukua upande na anaitumia ESCROW kujijenga yeye binafsi na siasa yake. Anatumia nafasi yake kama mwenyekiti wa PAC kufuta makovu ya kufukuzwa CHADEMA, huku akidhihirisha kuwa yeye ni muhimu kwa uhai wa upinzani nchini.
Zitto amefanikiwa kuonesha kuwa yeye ni muhimu kwa UKAWA, lakini pia ametumia nafasi yake ya uenyekiti wa PAC vibaya. Jambo hilo liliingiza bunge katika kufanya maamuzi kwa ushabiki wa vyama badala ya busara.
wasenge nyie na blog njaa yenu hivi kukutana na ukawa ni tatizo mbwa nyinyi
ReplyDelete