Alichokisema msichana aliyemtesa mtoto Uganda leo na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama

Unamkumbuka yule mfanyakazi wa ndani aliyemtesa mtoto nchini Uganda na kuteka hisia za watu wengi duniani? leo kesi yake imeweza kusomwa kwa mara nyingine.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe mwenye miaka 22 aliiambia mahakama nchini humo leo kuwa anajua kile alichokifanya na anakiri kosa hivyo anaomba watu wamsamehe kwa kuwa alifanya makosa.
Mfanyakazi huyo wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimpiga mtoto wa bosi wake ajulikanaye kwa jina la Arnella mwenye umri wa miezi 18 pia alikua akimkanyaga mtoto huyo bila huruma.

Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji, kiongozi wa mashitaka alimshitaki kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
Msichana huyo alikiri makosa yake na kuomba msamaha na Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani hapo licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo ypyote.
Kesi hiyo imeahirishwa tena hadi keshokutwa wakati hakimu akitarajiwa kutoa hukumu dhidi yake.
Binti huyo huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola za kimarekani 800 au adhabu zote mbili.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kama amekiri kosa wampunguzie adhabu au wamwache huru

    ReplyDelete
  2. Msamaha ndo kila kitu kama ameomba msamaha wamhurumie awe guru

    ReplyDelete
  3. Hakuna kusamehewa angemuua je?? Huyo binti pimbi nn mbona hakufikiria huko alipokuwa akifanya unyama wake!! Apewe adhabu kali ili iwe fundusho kwa wengine wenyewe tabia kama zake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad