AUNT EZEKIEL: Chagueni wenyewe ni Kitambi au Mimba

Japokuwa hadi sasa Muigizaji  Aunt Ezekiel Grayson anakanusha kuwa hana ujauzito, stori zake za kuwa na ujauzito zimezidi kuenea kwa kasi zaidi kwenye mitando ya kijamii na blogs mbalimbali za hapa BONGO.

Hii nikutokana na kuonekaana kwenye Klabu ya New Maisha iliyopo Masaki jijini Dar, Jumapili iliyopita akiwa ameshiba yaani kitumbo ndi huku akishindwa kukificha baada ya kila kitu kuonekana waziwazi kwa macho yasiyohitaki miwani.

KIGAUNI CHAANIKA KILA KITU                                      
Aunt, akiwa ukumbini humo na mastaa wenzake waliohudhuria kwenye shoo ya msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow anayesimamiwa na kampuni ya muigizaji, Wema Isaac Sepetu na Meneja Petit Man, alitinga akiwa amevaa kigauni cha drafti nyeupe na nyeusi ambacho kilionesha vilivyo tumbo lake.

AUNT ANASEMA AKANUSHA

Kwamujibu wa Global Publishers.info, Aunt  Ezekiel alikanusha na kusisitiza kuwa ni aina ya magauni anayovaa ndiyo yanayomuonesha na kitumbo lakini hana mimba.
“Sina huo ujauzito, labda ni kwa sababu ya aina ya magauni ninayovaa,” alisema Aunt kwa kifupi.

ALICHO-POST INSTAGRAM

Jana kupitia ukurasa wake wa instagram,Aunt Ezekiel aliweka picha yake akiwa tumbo wazi na kuandika ujume kuwa lazima tujue kutofautisha kati ya mimba na kitambi

Lazima ujue Kutofautisha kati ya Kitambi na Mimba Sasa hiki Chagueni wenyewe ni KITAMBI AU MIMBA!!!!!legoooooooooo.....

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad