Baada ya Diamond Platnumz kutua jijini Dar es salaam December 2 akitokea Afrika Kusini akiwa na tuzo zake 3 za Channel O, alikutana na wadau, mashabiki pamoja na waandishi pale Escape 1 kuzungumzia ushindi wake na safari nzima ilivyokuwa.
Miongoni mwa maeneo aliyozungumzia ni pamoja na umoja unaohitajika kwa wasanii wa Tanzania ili waweze kuwa wengi katika majukwaa ya kimataifa.
“Ombi langu mimi kiukweli ni moja tu, Unajua lazima kama alivyosema mheshimiwa hapa muziki wetu ushakuwa, watu wanaukubali na tushaona njia kama tunaweza so lazima sisi tujiamini wenyewe tusikaekae sana nyuma kwasababu watu kuna ile kuogopa cha kuona kama aah watanipokea kweli. Na zile za aah ntashindwa kuongea kizungu ntachekwa mi nishachekwa sana kwenye kizungu sana, lakini saizi naweza nikaingia hata Big Brother na broken zangu hivyo hivyo lakini napita hivyo hivyo nimeingia pale juzi Fally hajaongea mi nimeongea “.
Diamond pia ameendelea kuwaomba wasanii wenzake kutotengenezeana beef za wenyewe kwa wenyewe, na hakusita kumtaja Ally Kiba wakati akitoa mifano alipokuwa Nigeria na kujiona yuko peke yake hakuna msanii yeyote wa nyumbani zaidi yake.
“Kingine mimi nilikuwa nataka niombe tufute zile zama zakutengenezeana matatizo wasanii wenyewe kwa wenyewe wa Tanzania kwasababu haiwezi kutusaidia kabisa, alikuwa anaongea kitu mkubwa hapa, nilivyofika Nigeria nilikuwa najiona kama mkiwa kwasababu niko peke yangu, nikiangalia huku simuoni hata Jaguar, huku siwaoni wasanii wenzangu namtafuta Dimpoz namtafuta nani, hata Ally simuoni yaani niko peke yangu.”
Credit: BONGO5
Baada ya Kuchukua Tuzo Diamond Amchokonoa Tena Ali kiba
4
December 05, 2014
Tags
domo kumbuka kuna leo na kesho!! hata Kiba alipokuwa Marekani na Rkelly alikuwa peke yake!!
ReplyDeleteAMEONGEA UKWELI,WASANII FANYENI KAZI ACHENI KUTENGENEZA MAUGONVI YASIYO YA KICHWA WALI MIGUU,NEXT TIME TUNATAKA DOMO,ALLY,DIMPOZ,MDEE,LADY J,BARNABA WOTE MNAITWA KWENYE TUZO.
ReplyDeleteANONYMOUS KUWA MUELEWA,DOMO HAJAMTAJA ALLY KWA NAMNA MBAYA,NINYI NDIO WACHONGANISHI WA WASANII,KAZI YENU KUGEUZA TAFSIRI.
ReplyDeleteTatizo wabongo wengi ma mburura tunaendeshwa na hisia binafsi za kishabiki.diamond ameeleza jambo muhimu sana kwa wanamuziki wetu kuungana.amini usiamini tuna wasanii wenye uwezo mkubwa sana kuliko hata diamond lkn walishindwa kuzitumia fulsa.lkn diamond ameonyesha njia hivyo ni wakati wa kumtumia ili na wengine wafike huko.
Delete