Batuli: Mtunisi Hana Mvuto Kwangu, Nimepata Mzungu

Msanii ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa mwigizaji Nice Mohammed ‘ Mtunis ’ aitwaye batuli, amemchana zilipendwa wake huyo kwa kumwambia hana
mvuto!

Kuonesha msisitizo, Batuli alisema kwa Mtunis ilikuwa ni kama daraja tu , alishapita hivyo hana mpango naye tena kwani tayari amepata mchumba wa Kizungu , raia wa nchi moja barani Afrika, ambaye muda wowote atamtangaza kuwa mume wake .

Alisema anaamini kwamba si kila jambo lililowahi kumtokea lina maana kwake kwani hata kutoka na Mtunis ilikuwa ni kipindi cha muda mfupi na mchumba wake wa sasa ana mvuto zaidi kuliko zilipendwa wake huyo .

Akizidi kumwagia sifa mpenzi wake wa sasa ,Batuli alisema anajivunia kuwa ni mtu sahihi kwake, ni mfanyabiashara mkubwa kutoka nje na Bongo ana kampuni nyingine kubwa hivyo si mtu wa maisha duni kama wengine .

“Mtunis wapi bwana sasa hivi kwangu ? Hana mvuto na kama niliwahi kutoka naye basi kipindi kile , sasa hivi kiukweli nipo na wanaume ambaye nampenda na muda ukifika , ataniweka ndani, kila mmoja atamjua, ” alisema Batuli.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sijui wenzangu mnaonaje, ila nadhani hata mtunisi anajuta kutoka na mwanamke mshamba kama huyu. Kila issue yake lazima mtunisi awe mentioned dada ana kazi ya kutafuta umaarufu wa magazeti kwa nguvu. Hata movie moja siijui. Mama wewe tulia ulee watoto wako.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad