Kunyanyashwa kwa wasanii wa Kenya, kumemfanya Diamond na waandaji wa show yake ya Mombasa weekend iliyopita kutupiwa lawama na wapenzi wa muziki nchini humo.
Mtandao wa Standard Media wa Kenya, umeandika kuwa kwenye show hiyo iliyohudhuriwa na watu kibao, Diamond alitaka wasanii wengine wote waliokuwa watumbuize kwenye show hiyo na waliokuwa wamepangiwa kukaa naye kwenye VIP lounge, wakiwemo Susumila na Nyota Ndogo waondelewe.
Ilidaiwa pia kuwa Susumila na Nyota Ndogo walinyimwa maji ya kunywa na kwamba waliambiwa wanywe maji ya bomba kwakuwa maji ya kwenye chupa yalikuwa kwaajili ya Diamond peke yake.
Tukio hilo liliwafanya wasanii wa Mombasa waungane kuwalaani waandaji wa show hiyo ambapo VJ Delph alikataa kucheza muziki.
“Kama hili likiendelea, wapenzi wa muziki wa Mombasa watagomea show za Diamond mbeleni. Ni fedheha kwa wasanii wetu kutendewa hivyo nyumbani,” alisema Hassan Faisal wa Coastal Films.
From The Source:
The embarrassing treatment of Kenyan artistes has Tanzanian singer Diamond and an event’s organiser receiving backlash from music lovers. During a concert held in Mombasa over the weekend in which Diamond was the showstopper, the star demanded that all other artistes who had reservations in the VIP lounge, among them Susumila and Nyota Ndogo, be moved away. There was more drama after Susumila and Nyota Ndogo were denied drinking water. They were told to look for tap water as the bottled water was only for Diamond and his crew. The act saw Mombasa artistes unite to condemn the event organiser with VJ Delph declining to deejay.
Huo ndio umaarufu wa Platnumz!Hata siku moja 2mbili hawezi kukaa meza moja na chui!
ReplyDeleteUsilaumu kabla hujasikia upande wa pili, siamini Kama diamond anaweza fanya hivyo, labda walioandaa ndio waliobagua
ReplyDelete