KALI YA WIKI: Kwa iliyopita hii ndio ilikuwa kali ya mwaka kwa mwigizaji wa filamu Faiza Ally, kuvaa Diaper wavaayo watoto kuhifadhi haja zao maarufu kama ‘pempasi’ kwenye kusherekea siku yake ya kuzaliwa.
Tukio hilo lilitokea juzikati katika Hotel ya Sea Cliff iliyopo Masaki jijini Dar, ambako walialikwa watu wachache kwa ajili ya kula chakula cha jioni pamoja.
Faiza ambaye amezaa mtoto na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo atakuwepo kwenye kipindi cha TAKEONE, kwamujibu wa Zamaradi Mtetema ambae ndio muandaaji na mtagazaji wa kipindi hicho kinachorushwa na kituo cha televisheni cha CloudsTV saa tatu kamili usiku, Faiza leo ataeleza sababu za yeye kuvaa vile kwenye siku yake ya kuzaliwa, na alifikiria nini kufanya vile,na mengine mengi ikiwemo ameathirikaje baada ya kuachana na Baba Mtoto wake ambae ni Muheshimiwa Sugu!.
Faiza Ally ameshaigiza kwenye filamu kama TOUGH LIFE, WHY ME, JESCA, SECURITY na nyingine nyingi.
Sijui ilikuwa ni kutafuta kiki….tusubiri tusikie atasema nini!!
Faiza Kufunguka Kisa Cha Kuvaa Diaper (Pampers) Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa!!!!
0
December 24, 2014
Tags