Huyu Zari Vipi? Mbona Kamganda Diamond Hivyo..'Magazeti ya Uganda'

MITANDOA ya kijamii na vyombo vya habari vya Uganda vimemgeuka nyota wa vipindi vya runinga na Mwanamuziki Zari ‘The Boss Lady’ kwa madai kwamba amemganda mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz.

Gazeti la udaku la Red Pepper, mitandao ya ugvision.com, bigeye.ug na mingineyo, imedai kuwa nyota huyo amemganda mwanamuziki huyo tangu alipopata upenyo wa kurekodi naye singo jijini Dar es Salaam.

Mitandao hiyo ilimshambulia Zari kwa kumwambia kuwa kavuruga uhusiano baina ya Wema na mkali huyo wa video ya ‘Ntampata Wapi’, huku ikiponda picha ambayo Zari aliiweka mitandaoni ikimwonyesha akiwa na Diamond.

Mitandao hiyo imeponda kuwa Zari ana tabia ya kuwanadi wanaume anaotoka nao.

Wiki tatu zilizopita Zari amekuwa bega kwa bega na mwanamuziki Diamond, baada ya kutengeneza wimbo wa pamoja katika studio za Tuddy Thomas. Zari alionekana akipiga picha kadhaa na nyota huyo kabla ya kumsindikiza katika tuzo za CHOAMVA, Afrika Kusini na baadaye kurudi naye nchini.

Diamond ambaye alinyakua tuzo tatu za Channel O 2014, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla inayoandaliwa na Zari, ijulikanayo kama ‘Zari All White Ciroc Party’, itakayofanyika Desemba 18, mwaka huu.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zari mama tunakuomba utuachie kijana wetu coz tunaona UNATUBEMENDEA TU....!!!!!!!!!!!!!!!Jimama zima huoni ata haya kumvulia nguo kijana mdogo kama huyu wakulingana na mdogo wako wa 3!!!!!!! uwiiii naombeni msaada wadau nalemewhili mimi n then shame upon u SHUGA MAMY

    ReplyDelete
  2. Zari kula kwa raha zako diamond mwenyewe anapenda kubemedwa mbona wema naye mkubwa kwa diamond? kunyaa aje kuku bata kaharisha!!

    ReplyDelete
  3. Zali mtoto kakupendaje!!! wanawake kuolewa na wazee ndio naona sawa?? ila wanawake kuwa na vijana sio sawa?? mapenzi hayana umri kama mmependana kwa dhati miye nawapa 5

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad