Imebainika Kumbe Jack Patrick Alitwangwa Talaka Akiwa Jela

Na Imelda Mtema
Masikini! Wakati akiendelea kutumikia kifungo cha miaka saba jela huko Macau nchini China, mwanamitindo mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick, ametwangwa talaka na aliyekuwa mumewe, Abdullatif Fundikira ‘Tiff’ na tayari amemuoa Miss Tanzania 2011, Salha Israel.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita baada ya gazeti ndugu na hili, Amani kutoa habari ya Miss Tanzania kuolewa na mume wa Jack, Tiff alisema kuwa mke wake wa sasa (Salha) amemuoa kihalali na kwamba yeye siyo mume wa mtu kwa sababu ameshampa talaka Jack aliyemuoa mwaka 2011.

Kwa sasa mke wangu ni Salha. Sina mke mwingine zaidi yake kwa kuwa Jack nimeshampa talaka hivyo huyu mke wangu nimemuoa kihalali kabisa wala sina mke mwingine zaidi yake,” alisema Tiff.

Jack yupo selo tangu mwaka jana akitumikia kifungo cha miaka saba baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China akidaiwa kwamba kama atakuwa na heshima akiwa gerezani adhabu hiyo itapunguzwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad