Mtandao wa Instagram wiki hii umewapa majonzi baadhi ya watumiaji wake baada ya kufanya operation ya kufuta akaunti feki (spammy accounts ) na hivyo kuathiri namba ya followers kwa watu wengi.
Asilimia 18.9 ya akaunti (fake) za Instagram zimefutwa kuanzia Jumatano hadi Alhamisi.
“We’ve been deactivating spammy accounts from Instagram on an ongoing basis to improve your experience. As part of this effort, we will be deleting these accounts forever, so they will no longer be included in follower counts. This means that some of you will see a change in your follower count.” Wameandika Instagram.
Mastaa wa nje waliokumbwa na fagio hilo la followers ni pamoja na Justin Bieber ambaye amepoteza mashabiki (fake) milioni 3.5 sawa na asilimia 15 ya followers wake wote.
Mwingine ni Kim Kardashian ambaye amepoteza followers milioni 1.3 au asilimia 5.5 ya followers wake wote.
Rapper Mase ameamua kujiondoa kabisa Instagram siku ya Alhamis, muda mfupi baada ya kupoteza followers milioni 1.5
Instagram yafuta 18% ya akaunti feki, Justin Bieber, Kim Kardashian wapoteza followers zaidi ya milioni 4
0
December 19, 2014
Tags