Isabela Mpanda 'Roho Inaniuma Sana Ndoa Yangu na Luten Karama Imebuma Bila Kutarajia'

MSANII wa muziki Bongo, Isabela Mpanda amesema kuwa anasikitika kuona mwaka umeisha mipango yake ya kufunga pingu za maisha na mwandani wake wa siku nyingi Luten Karama imegonga mwamba na kutamani kuolewa ndoa ya kimyakimya. 

Akizungumza kwa masikitiko mwanadada huyo aliyewahi kutwaa taji la Miss Ruvuma alisema, maisha ya uchumba yameshamchosha na ndiyo maana anapigania kuolewa, ambapo harusi yao ilitarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, lakini kutokana na sababu zilizoshindwa kuzuilika ndoa imeshindikana hadi mwakani. 

Roho inaniuma sana natamani mno kuingia kwenye ndoa lakini kwa mwaka huu imebuma bila kutarajia, tulifanikiwa kufanya kikao kimoja tu cha harusi sasa nikafiwa na dada yangu ikabidi mipango yote isimame basi ndiyo kimya hadi sasa, nilimwambia Karama tuoane kimyakimya ndoa ya Bomani kisha sherehe itafuata akagoma, kwa hiyo tunatarajia kufunga pingu za maisha mapema mwakani Mungu akipenda,”alisema Isabela.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

  1. Huna sifa za kuwa mke wa mtu bado,karama anajifikiria kwanza maana ndoa si lelemama.

    ReplyDelete
  2. Usijali dada mungu atakujaalia utafika wakati wako utaingia kwenye ndoa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad