Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki(pichani) ameiagiza Halmashauri ya jiji hilo kuchukua hatua za haraka, kuziondoa kampuni zote udalali zinazokamata magari yanayovunja sheria za maegesho jijini humo.
Kauli hiyo ya Sadiki inakuja wakati kuna ongezeko la malalamiko ya wamiliki wa magari kuhusu kampuni hizo kuendesha vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji, ukatili na usumbufu hasa kwa wanawake huku kiongozi huyo akisema yamejaa ofisini kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, Sadiki alizitaja kampuni hizo kuwa ni Mwamkinga Auction Mart, Yono Auction Mart & Co Ltd na Tambaza Auction Mart & General Court Broker of the Tribunal.
“Utendaji wa kampuni hizi umeendelea kuwa kero kwa watumiaji wa barabara licha ya viongozi wa kampuni hizo kupewa maelekezo ya kuboresha huduma zao...Malalamiko niliyoyapokea ni mengi, hatuwezi kuvumilia yaendelee,” alisema Sadiki.
Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni kukamata magari kwenye nyumba za watu, kuwalazimisha wamiliki wa magari kuvutwa wakati gari linaweza kutembea lenyewe, kufukuza magari yanayodaiwa kuegeshwa vibaya na kusababisha ajali pamoja na kutoza faini viwango tofauti na vilivyoainishwa na halmashauri ya jiji.
“Unakuta magari mazuri na mazima yanavutwa na magari mabovu na kusababisha gari zima kuharibika. Lakini mbaya zaidi, faini halali ni Sh50,000 , wao wanatoza kuanzisha Sh200,000 hadi Sh500,000 . Hii ni kero ambayo hakuna mtu anayekubali.
Hata hivyo, kukamata magari kwa kuvizia mtu akiwa labda amepaki ananunua dawa au hata kushusha mgonjwa, wizi wa vifaa vya magari kwa baadhi ya magari yanayokamatwa... “Mtu anakamatiwa Kimara au Mwenge lakini anavutwa kupelekwa katika yadi yao Pugu au Kurasini, hii haivumiliki,” alisema Sadiki .
Aliongeza: “Wafanyakazi wa kampuni hizo wengi hawana weledi na wanafikiri mtu akishakuwa ‘baunsa’ anafaa na kwamba sehemu kubwa wamekuwa wakiwanyanyasa watu na kuwadhalilisha wanawake ambao hawawezi kupambana nao.”
Sadiki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema kuwa Halmashauri za Ilala, Kinondoni na Temeke zitachukua nafasi ya kampuni hizo hadi utaratibu mwingine utakapofuata.
“Nazishauri Halmashauri za Ilala, Temeke na Kinondoni kuigia mkataba na Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT ambao vijana wake wanaandaliwa kwa weledi na kufuata sheria za kijeshi na kuachana na wanaookotwa wasikokujua,” alisema.
Huku akisisitiza Sadiki alisema: “Ninawaomba radhi sana wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa matatizo yaliyokuwa wakiwakuta kutokana na kampuni hizo kuendesha mambo wanavyojua wao, licha ya kuwakemea mara tatu.”
"Yesterday's Pain Do Control Tomorrow's Potential"
Kampuni zinazokamata Magari Yanayovunja Sheria za Maegesho zafungiwa Baada ya Kuwa Kero Kwa Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
5
December 14, 2014
Tags
Safi sana Sadiki.
ReplyDeletesafi mkuu ,hao walikuwa waganga njaa
ReplyDeletebora maana hii mijitu inajifanyaga kama miungu vile. Bado manispaa ya dodoma na hicho kikampuni cha CONNECT na wafanyakazi wao wakiume waliojichubua kwa mikorogo ya jiki utadhani papai lililooza
ReplyDelete(k) (h) hongera sana Mzee Dar Es Salaam, mshauri na Mkuu wa mkoa wa Dodoma akifukuzie mbali hicho kikampuni cha Connect nacho.
ReplyDeleteHongera sana Mkuu, yaani ni shidaa!! Tena cha ajabu wako kuna mwanamke wanalazimisha kuingia ndani ya gari mbageini rushwa, yaani ni kero iliyopitiza, wakishavaa vishati vyao vya light blue mwanao na wamemaliza, halafu wafanyakazi wao wa kike wako kama changudoa, yaani ni keroo tena kipindi hiki cha sikukuu ndio kama wamelogwa. Kaza buti baba utuokoe wananchi wako.
ReplyDelete