Kijana Auwawa Kwa Kupigwa Risasi Akiwa Club Jijini Dar

Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja,  usiku wa kuamkia leo amepigwa risasi ya shingo na watu wasiojulikana wakati akiingia Club Maisha ilioko Oyster Bay jijini Dar es salaam. 

Tukio hilo lilitokea majira ya saa tano(5) usiku  ambapo kijana huyu akiwa na rafiki zake wanne(4) wakiwa ndio wanashuka kwenye gari yao waliyokuja nayo, walijikuta wamevamiwa na watu wawili wasiojulikana na yeye kupigwa risasi ya shingo kisha watu hao kutokomea kusikojulikana. 

Shuhuda wa tukio hilo alisema aliwaona watu wawili walioshuka kwenye gari ndogo nyeusi ilifunga breki kwa kasi kwani walionekana walikuwa mwendo kasi sana, kisha kuwavamia watu waliokuwa wanashuka kwenye gari ilikuwa imepaki muda mfupi baada ya kufika eneo hilo.

 shuhuda huyo aliendelea kwa kusema alisikia sauti ndogo ya kitu kilicholia "pyuuu!!!" bila ya kuelewa ni nini na kisha kufuatiwa na kelele nyingi za watu hao waliokuwa wamevamiwa. 
Waliotenda tukio hilo walitoweka mara moja eneo la tukio baada ya watu kujaa eneo ambalo kijana huyo alipigwa risasi alikuwa ameanguka chini. 

Polisi walifika eneo la tukio na kukuta kijana huyo ameanguka chini na damu nyingi zikiwa zimemtoka sehemu za shingoni na kifuani huku akiwa amewekewa nguo shingoni ili damu isiendelee kutoka ambapo ilisemekana ilikuwa ikitoka nyingi sana.


 Walimpakia kwenye gari yao kumuwahisha katika hospitali ya jirani ya mwananyamala, lakini kijana huyo alifia njiani akikimbizwa kuelekea hospitali.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. marehemu alazwe mahali pema peponi.amen!!!

    ReplyDelete
  2. Eeeeh!!!! Bongo sasa Holywood, huku kila club hata any parking lot ina camera Je hapo Maisha club kuna security camera????????? Meya wa jiji la Dar WAKE UP!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad