Kinachoendelea ktk Matokeo ya Serikali za Mitaa ni Mwanzo wa Mwisho wa CCM au ni Hasira tu za Escrow na Katiba?

Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanayoendelea kutoka, yanaonyesha CCM inaendelea kushindwa vibaya!, huku upinzani ukizidi kuwapokonya mitaa na vijiji!.

Kwa matokeo haya, inawezekana huu ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa CCM?!, au ni hasira tuu ya escrow na ile "bora katiba", hii huu kuwa ni upepo tuu na utapita na hali itatulia hivyo 2015, ni kama kawa?!, CCM ni ushindi wa kishindo?!.

Japo mwisho wa siku, the overall winner atakuwa ni CCM!, lakini kwa chama kilichokuwa kimeshika mitaa 100, kikaingia kwenye uchaguzi na kupoteza mtaa mmoja, kile chama kilichoshinda mitaa 99, na kupoteza mtaa mmoja ndio the losser, na chama kilichokuwa hakina mtaa, lakini sasa kimeshinda mtaa mmoja ndio the winner!.

Japo mpira ni dakika 90, na kutangulia sii kufika, kama ulivyo mwanzo wa ngoma ni lele, na mwanzo wa safari ni hatua!, inawezekana safari sasa ndio imeanza?!, Uchaguzi huu wa serikali za mitaa, mimi nauchukulia kama ni nusu fainali tuu, fainali yenyewe ni October, 2015!, kumbe ni kweli, "you can fool some people for some times, but you can't fool all the people all the times!". Inawezekana hii ya Wana UKAWA, ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa ule ukoloni na ukiritimba wa chama kimoja?, au ni nguvu tuu ya soda kwa hasira za escrow na "bora katiba?!.

Mpaka sasa siamini hiki kinachotokea!, kwa wale watu niliowaita Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!, kumbe hata ignorants, kunawakati wanafika mahali, ignorance yao inawatoka!. This is very surprising!.

kushinda ni kushinda tuu hata kama ni mtaa mmoja!, hii ni sweet victory!.

Na kushindwa ni kushindwa tuu, hata kama ni mtaa mmoja, kunauma!.

The winner takes it all, the looser standing small!.

Hongereni Washinda!, 

Poleni Washindwa!.

Pasco.

(Sina Chama, sina Upande!)
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. pumba tupu hakuna pointi yeyote hapa........

    ReplyDelete
  2. fikiri kwanza kabla ya kuandika haya ni mawazo mgando.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad