Tukiwa tunaelekea kuumaliza mwaka huu wa 2014 niameona sio mbaya nikawapa ubuyu huu, wa kile kinachodaiwa kuwa mwigizaji wa filamu za hapa bongo, Wastara Juma sasa hivi anatoka na mtangazaji na mwigizaji Bond Bin Sinnan.
Mbali na wawili hawa kuwa na mahusiano ya kizazi, kwani walishaigiza pamoja filamu kama “Uamini Fudhaifu” iliyotoka mwaka huu ambayo ina dhima ya mapenzi na vichekesho, inasemekana kwamba wawili hawa wameshavuka mstari na kutengeneza mausianao ya mtu na mpenzi wake.
Mitandaoni
Madai haya ya wawili hawa kuwa katika mahusiano yameanzia huko mitandaoni ususani mtandao wa Instagram, ambapo wawili hawa kwa mara kadhaa waneonekana wakipiga picha pamoja kwa mtindo wa “selfie” na kuacha maswali mengi kwa mashabiki wao ambao wengi wanauliza kunani? Lakini mara zote wamekuwa hawatoi majimbu. Hii ikapelekea watu wajiongeze kwa kuwaunga mkono na kuwatakia mahusiano mema na wengine wachache wakiponda.
Nilipozipata hizi, mzee wa ubuyu ni kaamua kuingia huko istagram kujionea, Ebwana ehh!!!.
Nilipopitia ukurasa wa Bond, nilikuta zaidi ya nusu za picha zake zote alizoweka ni zile amepiga na mwanadada Wastara au za wastara peke yake (baadhi hizo hapo juu)
Nikaingia kwa Wastara, huku nako nikamkuta, Bond na huko ndiko moto unapowaka wa wa wawili kukwa kwenye mahusinao kwani “comment” nyingi za mashabiki zinaonyesha kuwa hii ndio PROJECT mpya.
Bado wote wawili hawajasema lolote hadi sasa..sasa waswahili wansema, Lisemwalo?....
Kama ni kweli, Napenda kuwatakia kila la kheri, kwani ni jambo jema.
~By Mzee wa Ubuyu
via BongoMovies