Madai Mazito: Rose Mhando Atundikwa Ujauzito, Ajificha Ndani Kukwema Wadaku

STORI: Mwandishi Wetu
Haya ni madai mazito! Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando, anadaiwa kutundikwa mimba a.k.a ujauzito unaomfanya hivi sasa kutumia muda mwingi kujificha ndani, Risasi Jumamosi limenyetishiwa.

Mapema wiki hii, chanzo kimoja kilipiga simu katika chumba chetu cha habari na kusimulia kuhusu habari hiyo, kwamba, Rose ambaye hana mume, amenasa na muda wowote kuanzia sasa anaweza kuitwa mama.

KUMBE
Madai ya chanzo hicho yalieleza kwamba, staa huyo amekuwa akijichimbia nyumbani kwake mkoani  Dodoma tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa hakauki jijini Dar.

“Kama hamsadiki ninayowaambia, najua ninyi mmebobea kwenye habari za uchunguzi ‘so’ fanyeni yenu mtaniambia,” kilidai chanzo hicho kikiomba chondechonde kisichorwe jina gazetini.

KUJIRIDHISHA
Ili kujiridhisha na habari hiyo, pasipo kwanza kuwasiliana na Rose, moja kwa moja, gazeti hili lilimpigia simu mmoja wa watu wa karibu wa nyota huyo (jina linahifadhiwa), alipopatikana, aliulizwa kuhusu ishu hiyo na haya ndiyo aliyoyaeleza:

“Yaani hadi leo mlikuwa hamjapata hii habari? Mimi siku zote nilikuwa najua labda kwenu siyo habari kwa sababu ujauzito huu ni wa siku nyingi. “Hata sasa hivi ukimuona alivyo unajua wazi kuwa kuna kichanga tumboni kwani tumbo limechomoza hatari.”

Mtu huyo wa karibu alisema anapokuwa nyumbani Dodoma mara nyingi amekuwa mtu wa kukaa ndani tu kutokana na watu kumshangaa.Alisema Rose amekuwa akijificha kwa sababu ya kuogopa macho ya watu na uchovu unaotokana na hali aliyonayo ‘kuchoka’.

NANI MHUSIKA?
Juu ya nani mhusika wa mimba hiyo, mtu huyo wa karibu, ambaye anafahamu kila kinachofanywa na nyota huyo wa Wimbo wa Facebook alisema kuwa, inadhaniwa kuwa ni ya mcheza shoo wake (jina kapuni).

Inadaiwa kwamba, Rose, mara kadhaa amekuwa akisisitiza kuwa ni lazima amzalie mtoto jamaa huyo kwa jinsi anavyompenda.“Huyo mcheza shoo ana uhusiano naye kwa muda mrefu kidogo na ameshasema kwa watu wengi tu kwamba endapo Mungu atapenda basi atafurahi kama atamzalia mtoto.
“Mimi hajaniambia mimba hasa ni ya nani, lakini naziona dalili zote kuwa ni ya huyo kijana,” alisema mtu huyo.

MWENYEWE ANASEMAJE?
Baada ya kujiridhisha na maelezo ya mtu wake wa karibu, gazeti hili lilianza kumtafuta Rose, mama wa watoto watatu ambao wote amezaa na wanaume tofauti, lakini katika hali ya kushangaza, simu yake iliita hadi kukatika bila kupokelewa, hata baada ya kupigwa mara kadhaa.

Likiamini huenda alikuwa katika shughuli au mahali panapombana kuzungumza, gazeti hili lilimtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kumsomea mashitaka hayo ili atoe ufafanuzi, lakini pia hakuweza kujibu.

Likiamini huenda simu yake haisomeki kwa mtumishi huyo wa Mungu, gazeti hili lilitumia simu nyingine ambayo nayo iliita kwa muda mrefu hadi kukatika pasipo kupokelewa na hata pia alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu wenye maelezo kuhusu hali yake ya sasa, pia haukujibiwa hivyo jitihada zinaendelea.

NI MTOTO WA NNE
Endapo itathibitika, ujauzito wa Rose utakuwa ni wa mtoto wa nne ambapo mara kadhaa staa huyo amekuwa akisema hayupo tayari kuolewa hivyo kuwaacha baadhi ya watumishi midomo wazi wakiamini mtu wa sampuli yake haifai kuzaa nje ya ndoa.
GPL

"Yesterday's Pain Do Control Tomorrow's Potential"

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mi hili limama silipendi walitoe kwenye ulokole anachezea dini huyu mbwa, mara unga mara mimba halafu watu wanenyamaza tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. so what kwani ww ni msafi? kila mtu ana maisha yake ndo maana huendelei kwa kufuatilia maisha ya watu

      Delete
    2. Shes God's image 'akiwa binadamu' kumbe wewe wamuona mbwa! Mungu akusamehe bt mind you no one is holy under the sun. We live by the grace of the Lord she can repent and move on God is Mercyful

      Delete
  2. Sio aendelei ila elewa yy ni kioo cha jamii yampasa awe kivutio

    ReplyDelete
  3. Hapo issue ni watoto kupata matunzo na huduma zote muhimu kuzaa na wanaume tofauti haijalishi nani ni msafi asiyefanya hayo mambo na wapo mnaishia kutupa watoto au kutoa mimba au hata kwa kutumia condom bado issue inabaki umetenda lile tendo!!!

    ReplyDelete
  4. Kwa hivo kama ni kioo cha jamii huwa hana hisia?
    Kufikia sasa anaelewa wazi amekosea Mungu na hamna njia ingine ni kutubu na kumrudia Mungu na maisha na project ziendelee.huwa mwakosa kuelewa maceleb kwamba ni binadau mwenye uaweza kosa kama wewe na hata mwingine hiyo ni akili finyu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad