Huu ni wakati wa Yusuf Manji mwenyekiti tajiri wa Yanga anakiri kuwa zile bao 5 ambazo aliahidi kurid za Yanga kufungwa na Simba hali ni ngumu sana....ni wakati mwingine kabisa kwa unyonge anakubali kipigo cha bao 2 kwa nunge. "sisi washabiki wa Yanga tumechoka kufungwa na Simba tukijitahidi sana ni draw...maisha haya mpaka lini? " alizungumza juma jabiri mwenyekiti wa yanga tawi la huko manzese.... sikuweza kumuuliza mara mbili jina la tawi lake kwa kuwa alionekana mwenye hasira akitokwa mate huku jasho likimtoka. labda huu ni wakati wa YANGA kujiangalia sana namna ya uendeshaji wao wa Team kwa kutumia Magazeti. hili ni moja ya tatizo kubwa walilonalo Yanga kwa kuewekeza sana kwenye magazeti kuipamba yanga lakini wanapokuja uwanjani huwa wanacheza mpira wa kawaida tu. Yanga ni moja ya team kubwa sana baran Africa inapaswa ijiangalie namna ya kuweza kuwa na team bora ambayo itasajili wachezaji wenye uwezo na si wale wachezaji ambao Simba ilionesha kuwataka....tumeona namna Simba inavyowasababishia Yanga wasajili hata wachezaji wabovu kwa vile tu huwa inajifanya wakati mwingine kutaka kuwafanya yanga wasajili mchezaji ambaye wao wanajifanya kuonesha nia ya kumtaka.
"Yesterday's Pain Do Control Tomorrow's Potential"