Jana Kwenye Mitandao zimezagaa Habari Kuhusu Huyu Dada aliyepigwa Risasi Maeneo ya Morocco nyuma ya Airtel Building a lady was shot to dead!!
Bodaboda walivamia kiduka cha M-PESA, tiGO PESA na Airtel Money; wakati wanaondoka wakawa wanapiga risasi ikampata huyu dada alikuwa anajipitia barabarani hajui hili wala lile.
My Take:
Dah! Kwa mambo kama haya ndio najikuta naamini kwamba Kuwa Mtanzania ni shida sana, yaani hawa wahuni wanaenda kupora kwenye M-Pesa na kuua watu halafu wanafanikiwa kuondoka wakiwa salama? Yako wapi mafunzo ya Jeshi la Polisi, waliokaa CCP Moshi kwa miezi sita kwa kodi za wananchi?
Uko wapi ujasiri wa Polisi wanaopandishana vyeo kila kukicha? Wahuni wanaua wananchi mchana kabisa na bado mnasema hii ni nchi ya amani? Imekuwa polisi ya maneno mengi tu na vitendo vifupi. Yaani nimejisikia vibaya mno kwa kifo cha huyu mama ambaye alikuwa akipita njia tu na zake. (RIP)
Mpita Njia Auwawa kwa Risasi na Majambazi Waliovamia na Kupora Duka la MPesa Morocco
1
December 24, 2014
Tags
Kweli mafunzo ya miezi 6 haitoshi kwa usalama wa raia na mali zao,wanatakiwa elimu ya kutosha,masomo kuhusu jamii,sheria za nchi,jinsi ya kujihami self defence,kujifunza first aid and CPR,ili kuweza kuokoa maisha ya watu,kutalii nchi 3 au 2 kabla ya kuajiriwa,Mungu tusaidie ,katiak nchi yetu Tanzania,pia askari wawe wavumilivu.
ReplyDelete