Mshindi wa pili wa BBA Hotshots, Tayo kutoka Nigeria amekanusha ripoti zilisambaa wiki hii kuwa amezawadiwa $350,000 na bilionea wa Nigeria baada ya kuzikosa $300,000 za BBA zilizonyakuliwa na mshindi wa kwanza mwaka huu Idris wa Tanzania.
Ripoti hizo zilidai kuwa Tayo alipewa zawadi hiyo na bilionea aitwaye Ayiri Emani kama kifuta jasho au fidia ya kuzikosa $300,000 za mshindi wa HotShots.
Tayo amekanusha habari hizo alipohojiwa na kituo cha Radio 1 South Africa. Amesema kuwa habari hizo za kuwa amepewa kiasi hicho kikubwa cha pesa na huku hata hamfahamu bilionea huyo, zimemletea usumbufu kwasababu watu wengi watadhani yeye ni milionea na huku sio kweli.
Tayo aliongeza kuwa yeye na Idris ni marafiki na anatarajia kuja Tanzania mapema iwezekanavyo.
Chanzo: Big Brother Africa 2014
Mshindi wa Pili wa BBA Hotshots 2014: Akanusha kupewa pesa na tajiri wa Nigeria
1
December 14, 2014
Tags
ukweli ni mzuri hadi rahaaa sasa bilionea naye atafutwe na aulizwee kabisa katoa mpunga au laa! ni ruzuku au escrow aelezee vizuri asee.
ReplyDelete