Mtani Jembe Yazua Balaa Yanga..Waamua Kumfukuza Kumtupia Virago Kocha Maximo

Baada ya kuchapwa mabao 2-0 na mahasimu wao wa soka Simba SC katika mchezo wa ‘ Hisani Nani Mtani Jembe’ siku ya Jumamosi iliyopita, klabu ya Yanga SC imeamua kufikia maamuzi magumu ya kumfuta kazi kocha Marcio Maximo na ni wazi Mholanzi, Hans Van De Pluijm atachukua nafasi hiyo. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kumfukuza kazi kocha wao mara baada ya kufungwa na Simba. Ikumbukwe mwaka uliopita, Mholanzi, Ernie Brandts aliondoshwa baada ya kufungwa mabao 3-1 katika Mtani Jembe.

Tofauti na ilivyokuwa kwa Brandts ambaye aliifundisha Yanga kwa mwaka mmoja na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/13, Maximo yeye amefukuzwa baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo tisa ndani ya miezi mitatu. Yanga imepoteza michezo miwili kati ya saba ya ligi kuu msimu huu, Maximo ambaye alianza vizuri klabuni hapo kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii, alipoteza mchezo wa kwanza tu wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Yanga imeshinda michezo minne msimu huu, lakini hadi l,igi inasimama katika raundi ya saba hakuna mtu alikuwa na shaka kuhusu uwezo wa Maximo. Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amechokwa haraka sana na mashabiki, wapenzi, wanachama na viongozi wa klabu yake kutokana na kiwango kidogo cha uchezaji. Mifumo yake ya ufundishaji imekosa mvuto, lakini kitendo cha kufungwa kidhaifu na Simba kimeshindwa kuvumilika.

COUTINHO, JAJA, EMERSON WAMPONZA?
Ndiyo sababu kubwa, ukitoa mbinu zake, Maximo alikuwa akiwakumbatia zaidi wachezaji raia wa Brazil, Andrey Coutinho, Geilson Santos ( ambaye aliomba mwenyewe kuachwa baada ya michezo saba), kwa Emerson Oliveira siwezi kuzungumzia kwa sababu mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo alicheza katika kiwango cha kawaida wakati alipoichezea Yanga kwa mara ya kwanza.

Jaja alifunga mara mbili dhidi ya Azam, ila alikosa makali katika ligi kuu kiasi cha kufunga bao moja tu katika michezo saba ya ligi kuu. Alishindwa kumudu presha ya mashabiki wa Yanga ambao hawakuwa wakipendezwa na kiwango chake huku uchezaji wake wa taratibu ukiwaboa wengi. Maximo aliwanyima nafasi washambuaji kama Said Bahanunzi, Jerry Tegete, Saimon Msuva, Hussein Javu na Hamis Kizza hata pale wachezaji hao wa Kibrazil waliposhindwa kufanya vizuri.

Kuwang’ang’ania wachezaji hao na kuwanyima nafasi wale wenye uwezo kumewakera . Brandts aliondolewa baada ya kufungwa 3-1 licha ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili zaidi, yeye aliondolewa kwa kuwa alipingana na uamuzi wa viongozi kuwasajili baadhi ya wachezaji ambao hakuwataka wakati ule.

Brandts ndiye mwalimu aliyeifanya Yanga kucheza mchezo mzuri wa kupasiana na ndiye aliyeimarisha kiwango cha wachezaji kama, Saimon Msuva, Frank Domayo ( yuko Azam FC kwa sasa), Juma Abdul, Oscar Joshua na wengineo lakini kwa Maximo imekuwa ni tofauti, wachezaji wengi wameshuka viwango na ameshindwa kuwaimarisha wachezaji ambao ‘ wanasua-sua’. Yanga wamefanya uamuzi sahihi kwa kumuondoa Maximo na Coutinho.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa na safi saana,Maximo mbishi sana,anataka analopanga yeye ndilo liwe,hataki ushauri wa mtu mwingine.Japokuwa kufungwa ni sehemu ya mchezo lakini hao wabrazil wake aliokuja nao wamechangia sana.Aende tu.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad