Hili halikuwepo miaka ya 90s kurudi nyuma, sisemi kwamba haikuwa ikitokea, la hasha! bali hata kama ilikuwa inatokea basi ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na ilivyo sasa.
Katika maeneo ninayokuwa hasa kwa watu mbalimbali ninawafahamu, jambo hili linaonekana kukuwa zaidi ya mara dufu na inavyoonekana hali ikazidi huko mbele ya safari.
Mabinti wengi wanaozaa wakiwa bado hata hawajaposwa wamekuwa wakiwaacha watoto wao wakilelewa na babu&bibi huku wakiendelea masuala yao ikiwemo kuendeleza uhusiano na wanaume ambao unapelekea kuongeza idadi ya watoto kwa wazazi bila kujua ugumu wa kulea watoto.
Wanaume wamekuwa wakiwazalisha mabinti bila kuwaoa wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kulea badala yake mwanamke ndio anaachiwa jukumu la uangalizi wa mtoto ambaye naye anakabidhi majukumu kwa wazazi wake! kimsingi wazazi hawawezi kuwakataa watoto wa watoto wao.
Suala linaonekana kuwa mzigo hata kama mtoto atapewa mahitaji mengine kama kulishwa na kuvishwa kwa gharama za nje ya wazazi wa binti lakini suala la kuwaangalia watoto ni zito na linachosha maana linaonekana kuwasumbua wazee tu ambao jukumu lao la kuangalia watoto lilishapita tangu siku nyingi nyuma.
Shida Iko Wapi Jamani?