Pancho Mwamba Afunguka Kuhusu Issue ya Kufumaniwa na Kuchukua Kichapo

Stori: Erick Evarist
Vunja ukimya! Mwanamuziki mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeitumikia Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ya Bongo, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ ameibuka na kufungukia skendo ya kufumaniwa iliyosambaa kwa kasi kama moto wa kifuu, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.

Wikiendi iliyopita, uvumi wa Patchou kufumaniwa uliibuka na kusambaa mitandaoni kufuatia kuwepo kwa picha iliyomuonesha akiwa amevimba usoni hususan katika maeneo ya macho na mdomoni.
Watu mbalimbali mitandaoni, walitumiana picha hiyo huku wakisindikiza na ujumbe wa mtu aliyeiposti awali na kuandika kuwa mwanamuziki huyo amevimba baada ya kufumaniwa na kutembezewa kichapo cha mbwa mwitu.

Wakati Ijumaa Wikienda likiwa katika harakati ya kuchimba ukweli wa jambo hilo (kawaida ya Global Publishers), mwanamuziki huyo alitinga katika ofisi za gazeti hili na kutumia dakika 30 kuanika ukweli kuhusiana na uvumi huo.

“Nimesikitishwa sana na jambo hili. Sijafumaniwa chochote, watu tu wameamua kunichafua. Mimi nina ‘aleji’ na pombe, kuna dawa nilishauriwa niwe nakunywa kila ninapotaka kunywa pombe.

“Sasa bahati mbaya siku hiyo nikalazimisha kunywa bila kutumia dawa, uso ndiyo ukavimba namna ile. Sasa nilijipiga picha usoni nikaposti Instagram na kuwaomba watu ushauri kama wanajua tiba ya ugonjwa wangu wanisaidie, nikashangaa ghafla watu wakaisambaza picha hiyo na vichwa vyao tofautitofauti, imenisumbua sana,” alisema Patchou huku uso wake ukiwa umerudi katika hali yake ya kawaida.

Mhariri-Kuna kila sababu ya serikali kupitia Wizara ya Sayansi na Teknolojia kulitazama kwa jicho la tatu suala la watu wanaokurupuka na kuposti picha sizizokuwa na ukweli au ukiukwaji wa maadili maana tatizo hili linazidi kushamiri kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad