Rais JK Hashinikizwi, Anaamua kwa Maslahi Mapana ya Nchi

Nimegundua Jk ni rais ambaye hakika Watz hatutomsahau na hatupaswi kumsahau, ametoa uhuru hata wa kumtukana akakaa kimya,wa kumshinikiza na bado akawa calm,wa kujaribu kuichezea na kuijaribu serikali yake na bado akakuvumilia. Neno moja kwenu nyie vibaraka wa wasaka U-rais, wafanyabiashara madalali na wengine wenye kariba ya kutotaka kuona mwenzio anaweka historia ya kuitumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa,wakati Rais Kikwete anaingia madarakan ni asilimia 6 wa wananchi wote walokuwa wanapata umeme,leo hii Watz asilimia 35 wanaaccess na umeme hasa vijijini, barabara za rami ameongeza kwa asilimia 25 network ya barabara za rami, huduma za afya karibu kila kijiji kina zahanati na kila kata kuna kituo cha afya na mengine mengi, juzi nimepata kusikia tunafanya vizuri katika kupambana na rushwa. Ila siwalaumu sana ila ndo tulivyo na itabaki kama challenge kwa rais ajaye, ila kwa ufupi serikali hii imejitahidi sana tena sana but one word kwenu vibaraka, mipango yenu na mabeberu wa magharibi inajulikana na mtashindwa
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Raisi lazima akosolewe pia, hayo ni madaraka amepewa na raia kwa kuchaguliwa, kama demokrasia, na lazima atekeleze wajibu wake, kwanini asikosolewe wani yeye siyo binadam hakosei, atendi yasiyo takiwa, huko marekani Obama mwenyewe kila siku anakosolewa, anchorwa, anatukanwa, tena uhko kwa wenzetu ujinga kama huu wa kuiba kodi au mslahi ya nchi looo!!!! awautaki na wala hawatakuacha kamwe...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad