Msanii wa muziki wa Bongofleva Ray C ambaye amekuwa katika wakati mgumu kwa kipindi kirefu kuingia katika matumizi ya madawa ya kulevya amekuwa akijitahidi sana kuwashawishi vijana kuhusiana na vita dhidi ya matumizi ya madawa hayo.
Ray C amesema kuwa tangu alipokuwa akipatiwa matibabu katika taasisi inayoshughulika na waathirika wa madawa hayo, bado amekuwa akipata mtazamo hasi kwa baadhi ya watu kutokana na yeye binafsi kuwa mhanga wa matumizi ya madawa hayo na Baadhi ya watu kuwa wagumu wa kuukubali ukweli hivyo kumuona yeye kama adui ...
Mara Kadhaa Ray C ameingia katika mikwaruzano ya hapa na pale na Wasanii Kama TID na Chid Benzi ambao kuna tetesi kuwa wanatumia vilevi hivyo pale anapojaribu kuwashauri kupitia mitandao ya kijamii kuacha Matumizi ya Dawa hizo.
Je unamshauri nini Ray C kuhusu vita dhidi ya Matuzi ya Madawa ya Kulevya ?