Tibaijuka: Kwakuwa Rais Ametengua Uteuzi Wangu, Sasa Nipo Jimboni Natatua Kero za Wananchi

Wananchi mkoani kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani waziri wa ardhi nyumba na makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.

Wakiongea na ITV wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua nini hatima ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk. kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri wengine waliohusika katika sakata hilo na kumuuondoa waziri Tibaijuka napia wamebaki na sintofahamu ambapo wamemtaka Rais kutoa ufafanuzi kuwa licha kumg’oa madarakani kiongozi huyo Je, Pesa hizo zitarudishwa kwenye akauti hiyo ya TEGETA ESCROW au la.

Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa kagera Hamimu Mahamudu amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa jana wakati akiongea na wazee wa jijini Dar es salaam kwa kumuondoa kiongozi huyo huku katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema katika manispaa ya Bukoba Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa Pesa za Escrow zitarudishwa lini katika akanti hiyo au kuwaondoa viongozi hao madarakani ndio suluhisho la kwamba pesa hizo hazirudishi?.

Kwa upande wake aliyekuwa Waziri wa ardhi nyumba na makazi Profesa anna tibaijuka amesema licha Rais kumuondo katika nafasi yake aliyokuwa nayo sasa amerudi jimboni kwake kwaajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba Pesa hizo alipewa na lugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa hizo zilitoka katika akaunti ya TEGETA SCROW ndomaana hakutaka kujiuzulu mapema.

Chanzo:ITV
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eti cheo nilichokuwa nacho nilishindwa kutatunua maisha ya wananchi jimboni kwangu sasa ninaweza kuyatatua,really?hivi huo uprofesa walipewa wapi?Kwa nn uliendelea kuwa mbunge wakati ulijuwa cheo cha uwaziri kinakukaba kuwasaidia watu jimboni kwako.?au ndio sizitaki mbivu hizi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kunywa soda hapo kwa Mangi,choma mguu wa mbuzi pia,
      natuma pesa kwa mangi kwa m-pesa.

      Delete
    2. Umenena mdau.Hata huku jimboni anakosemea amejichafua na hata akitumia hizo hela za ESCROW kutununua/Kutupoza tutapokea na hapati kitu.Hatapata ushirikiano.

      Delete
  2. Sasa mama ndio anakumbuka kurudi jimboni kwake na kwenda kuwatatulia matatizo hao wadanganyika wa huko, siku zote alikuwa hayaoni matatizo yao sasa anataka akawadanganye ajisafishe, kuwa yeye ni mwadilifu...hayaaa kwa wadanganyika poa tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad