Binafsi nimekuwa nikifuatilia hili suala la Diamond kuwa na msuguano na Davido tokea ushindi wa Idris Big Brother na nikiri kuwa Diamond hakupaswa kusema aliyosema dhidi ya Davido kwa sake ya urafiki wao!
Kwanini nasema hivyo? coz thamani ya urafiki waliokuwa nayo haiwezi kupotezwa kirahisi hivyo ingawa kuna watu wanafurahia tena kwa sababu za kitoto, kwa wale walioishasoma novel ya godfather nadhani wananielewa ninapozungumzia thamani ya urafiki! Kwani urafiki ni kama kula tunda na ukimaliza kuipanda mbegu yake ili siku utakapohitaji tena tunda uwe na sehem pa kulipata.
Sasa ninachoona ni giza kubwa mbele yetu sie mashabiki wa Diamond hatuoni ukweli tumejikinga kwenye kivuli cha uzalendo, hatutaki kukubali kuwa Davido kasaidia kupush mafanikio ya Diamond kwa kiasi fulani, mara baada ya number one rmx kutoka milango ilianza kufunguka kwa kasi kwa Diamond na hili wengi hatulioni bado tumefunikwa na kivuli cha uzalendo hatusimami kwny fact! ukitaka kuamini hili nenda youtube kaangalie number one rmx imeangaliwa na watu wangapi dhidi ya original version!
Kwa taarifa yako kuna gape la watu zaidi ya million mbili. Ndyo tunakubal Davido siyo mungu so Diamond hana haja ya kumtetemekea lakini kwa hili alipaswa kuonyesha heshima angalau kidogo kwani alichofanya ni ukosefu wa fadhila wa hali ya juu. mwisho na suggest Diamond afanye mpango amalize hili suala hata kama ni kimya kimya ili kuondoa tension iliyopo sasa.
Tunapoficha makosa ya Diamond kwa kisingizio cha uzalendo
8
December 11, 2014
Tags
Tatizo Diamond atalimaliza kwa kiingereza gani na Madame washatemana? Bi mkubwa Zari nae hawajashibana kiivo hadi aanze kum kompozia email...Msameheni bure jamani.
ReplyDeleteDiamond ana matatizo makubwa zaidi ya yale ya Davido.
ReplyDelete(1) Baada ya kumfuata Davido huko kwao Nigeria akasaidiwa kutoa remix ya wimbo wake ambayo ilivuma sana kuliko origino yake. Aliskika akitamba kuwa amemsaidia Davido kujulikana. Hiyo ilikuwa ni kosa ambalo sijui nani asiyeliona, kwa vile siyo Davido aliyeomba saidiwa kujulikana bali ni yeye Diamond.
(2) Kwenye BET awards wakati Davido anahsinda, aliwakariobisha wasanii wote wa Afrika ajumuike naye jukwaani, lakini Diamodn akakataa. Hiyo ilikuwa ni tabia mbaya sana kwa diamond kufanya mbele ya jumuia ya kimataifa.
(3) baada ya davido kuandika kuwa they cheat again, kabla hata hatujajua alikuwa ya maana gani, diamond akaandika kutoa tafsir ya kucheat kuwa maana ya ushindi. Hapo ndipo akasabisha mambo kuwa spiralled out of control. Nakumbuka nilimtumia twitt ya kushauri awe na diplomacy sijui kama aliisoma kwa vile yeye ni staa na anapata message nyingi sana. Bila diamond kuweka maneno yake, jambo hili lingekwisha bila matatizo na huenda tungefahamu kuwa cheat aliyokuwa akizungumza Davido ilikuwa na maana gani.
Diamond ana tabia ya kutjipima na mtu na baadaye akamdharau. Kuna mwandishi alieandika makala moja leo akionyesha jinsi Diamodn alivyokuwa na kiu ya kujipima na Ali Kiba lakini akapewa Chameleone, halafu baadaye akaanza kumponda Kiba.
Nyota yake Diamopnd ni kubwa lakini akumbuke tena kuwa aliyempa kiti ndiye aliwapa wengine kumbi, anapopanda mlimani awasalimiea anaokutana nao kwani ataweza kukutana nao tena wakati anatelemka
Atakubali vipi huo ushauri wako wakati waliomzunguka sasa hivi ni Zero brain? Washauri wake wakubwa wameshalifanya hili jambo ni issue ya kimataifa, kwa mfano kulikuwa na haja gani yule shemeji yake blogger kulikuza hili swala kwenye blogu yake? Na huyo Mwanamke wa Kiganda nae atamshauri nini? Sana sana atazidi kuonyesha dharau tu, angekuwa bado yuko na yule mwanamke mwepesi wa kusamehe na kusahau asingelifanya hayo kwa sababu marafiki wanaokuzunguka wanachangia katika kufanya maamuzi fulani fulanu.
ReplyDeleteUstaarabu hauuuzwi dukani mtu huzaliwa nao asifikiri hapo alipo ndio amefika mwisho kama suala la kupata award ya Channel O mbona hata Witness Rapa wa kike wa kufokafoka aliyekuwa anaimba na Shaa nae alishapata hiyo award siku nyingi zilizopita, yuwapi sasa? Nani anamjua tena kama alikuwa juu.
tatizo la domo keshavimba kichwa, na hajui nini haswa kiko nyuma ya mafanikio yake, yeye anafikiri huu mziki wake anaoimba ambao hauvuki mbali ya Afrika mashariki, bila dovido mziki wake ungeishia humu humu, kenya, uganda na Tanzania, kwanza domo arepresent how a Tanzania person dress or act, watanzania mila zetu atuvai kata mkundu wala mahereni.
ReplyDeletei'm a big fan of diamond but man what he did is not right at all,he definately need to apologize
ReplyDeleteni kweli kabisa, kwanza mi naamini bado davido hakuturushia dongo sisi watz kua tume cheat dat dongo wan kwa awo waandaji wa BBA, ila watz tulidandia tren kwa mbele tukaona ni sie!! ataa kama ni kweli diamond hakutakiwa kua mkosefu wa fadhila namna ile haswa baada ya kuona fans wake na watz wengine waliouzika na status ile ya davido alipaswa akitulize, kama anazani amefika mi naona ndio kwanza safari inaanza kwa hali inavoendelea nani atataka kufanya kazi na sie wakosefu wa fadhilila tusiojua kujibu hoja kwa hoja badala yake hoja kwa matusi ya nguoni....daimond anapaswa akitulize tu c vyenginevyo
ReplyDeleteJamani mliona nyapu isiosheviwa?Zari nimemdharauuu
ReplyDeleteNadhani mlichompa ni kikubwa sana km ni muelewa ataelewa na kufanyia kazi ila km anajiona yupo juu hawezi kujishusha sisi mashabiki tupo tunamsubiri iko cku atashuka hawezi kaa milele,aheshimu kila mmoja.
ReplyDelete