Katika ripoti iliyotoka jana kuhusu utafiti uliofanywa na Economists Intelligence Unit ya nchini Uingereza, ndugu Edward Lowassa kaongoza tena katika utafiti huo. Sehemu ya ripoti hiyo inaeleza ya kwamba Lowassa ndiye mwanasiasa anayekubalika zaidi ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwania urais 2015.
Economist Intelligence Unit ni moja ya taasisi/kitengo bora duniani katika maswala ya kiitafiti kwenye nyanja mbali mbali likiwemo maswala ya uchaguzi.
Tarehe 26/11/2007, kitengo hiki kilitoa ripoti ya utafiti wao kuhusu uchaguzi wa Marekani ya kwamba Obama ataibuka mshindi katika uchaguzi wa 2008. Matokeo nafkiri tunayajua....
Tarehe 14/10/2012, kitengo hiki hiki kilitoa ripoti kuhusu uchaguzi wa nchini Ghana, ya kwamba John Mahama ataongoza katika uchaguzi huo na ndiye alikuwa chaguo la wananchi. Matokeo wote tunayo....
Tarehe 24/10/2014, kitengo hiki hiki kilitoa ripoti kuhusu uchaguzi wa nchini Brazil. Katika ripoti hiyo mgombea Dilma Rouseff aliibuka mshindi kama kitengo hicho kilivyotoa ripoti yake ya kiutafiti..
Jana tarehe 20/12/2014, kitengo hicho kimetoa ripoti ya utafiti kuhusu uchaguzi wa mwakani hapa nchini. Na kumpa Lowassa ushindi mkubwa sana...
Mytake: chonde chonde tusithubutu hata kidogo kutupilia mbali maoni ya wananchi. Uchaguzi wa 2002 nchini Kenya, chama cha KANU kilipuuza maoni ya wananchi na hatimaye matokeo leo hii tunayo vichwani mwetu. Sauti ya wananchi ni kubwa sana ingawa unaweza usiione mpaka pale utakapo pata pigo takatifu.
Huu ni utafiti wa tatu mfululizo unaowagusa wananchi. Ni wito kwa CCM kusoma alama za nyakati na kusikia sauti za wananchi. Kura za maoni ni sauti za wananchi.
Source: magazeti ya leo (Mtanzania)..
Asante
Ocampo four