Zitto Kabwe ni mwanasiasa mwenye thamani ya juu katika siasa zetu za Afrika,mwanasiasa huyu ameonesha ubora wake katika suala zima la kupiga vita ufisadi na kusimamia maslahi ya Taifa.Zitto Kabwe huyu kaweka rekodi kubwa ambayo haijawahi fikia na mwanasiasa yeyote hapa nchini katika kuzisimamia ajenda nyingi na kufika nazo mwisho kwa maslahi ya taifa na amekuwa ametulia na asiyependa kukurupuka.
Thamani ya Zitto Kabwe nayoisema na wenye kuijua wanaanza kuithamini na kuitumia ni uamuzi wa Profesa mchumi wa hali ya juu Ibrahim Lipumba kuamua kuitumia thamani ya mwanasiasa huyu kwa kumpa mwaliko wa nguvu katika ziara zake za mtwara chini ya chama cha Cuf.Cuf itumieni thamani hii kwa kumtumia mwanasiasa huyu kwa mabadiliko ya kweli kwa wanamtwara.Wanamtwara jiandaeni kwa kupata somo la nguvu na mabadiliko ya kweli kutoka kwa mwanasiasa wa mabadiliko Zitto Kabwe.
Mabadiliko ya kweli yanaletwa na watu wenye dhamira ya kweli na sikuzote Mungu hawatupi.
Hansen Nasli