Wema Sepetu na Mpambe Wake Wafunguliwa Kesi na Kupandishwa Kizimbani

Mwigizaji wa filamu za kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kujibu kesi ya kushambuliwa vijana wawili, Rashid Balazi na Juma Bushiri, wakazi wa jijini Dar, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.

Katika kujibu kesi hiyo, Madam Wema hatakuwa peke yake kwani mpambe wake, Petit Man naye anahusika katika kesi hiyo kwa kuwa ndiye mshtakiwa wa kwanza.

Hivi karibuni kabla Madam Wema hajasafiri kwenda nchini Ghana kufanya kazi na staa wa huko, Van Vicker, Petit Man alidaiwa kuhusika kuandaa mchezo mchafu wa kuwateka na kuwashushia kipigo cha mbwa mwitu Rashid na Juma, tukio ambalo lilichukua nafasi nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.

Ilidaiwa kwamba, Petit Man alipoteza simu na kuwahisi vijana hao ambao mmoja wao alikuwa ni fundi bomba, ambaye alikuwa akitengeneza bomba nyumbani hapo.

Walivyowa-Tembezea Kichapo

Baada ya kuwabana vijana hao na kutotoshelezwa na majibu yao, ilidaiwa kwamba Petit Man, kwa kushirikiana na Wema waliwaita vijana wa kihuni ‘mbwa mwitu’ na kuwafungia nyumbani kwa Wema kisha kuwapa kipondo ‘hevi’ ili watoe simu hiyo lakini hadi dakika za mwisho walikataa kuwa hawakuchukua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad