Zamaradi Mketema Atoa ya Moyoni Kuhusu Bongo Movies 'Kwanini Mmeridhika Hivi' Atamani Atokee Kanumba Mwingine

Leo mwanadada Zamaradi mketema ameamua kusema haya kuhusu filamu zetu nchini. Kama wewe ni mdau wa bongo movies tafadhali tusaidie kutoa maoni yako juu ya maswali haya ambayo zamaradi anauliza…

Hichi ndicho alichosema…

“…Natamani sana siku moja atokee mtu kwenye hii sekta atutambulishe hata kama sio kimataifa basi africa tu... R.I.P KANUMBA alianza kuonesha mwangaza na juhudi binafsi zilionekana na kila mtu aliona huenda angefika mbali.. lakini baada ya hapo sioni tena!!!!

Mbona hapa nyumbani ni wakubwa tu..? Nini kinawakwamisha..?  Kwanini wasanii wetu wa filamu ukubwa wao unaishia nyumbani tu....!!? Tatizo ni nini!!!????? kiukweli ni kama inakatisha tamaa na inaonekana kabisa watu wamerelax na ustar wa bongo wakati wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi... wana bongo movie tukifika kwa wenzetu unaona kabisa tunapwaya kiasi gani.. Ujanja wetu ni nyumbani tu!!?? why!!!?? tukianza utanzania wa kufichaficha tutasifiana uongo lakini tukiwa wakweli na nafsi zetu tutaliona hilo na kuchukulia kama challenge..!!! ukweli ni kwamba hii tasnia inasikitisha!!! tena sana.. nahisi sasahivi tunafanya filamu kwa ajili ya nyumbani tu na tukiingia kwenye mabendi tukisharushwa tumeridhika!! kweli!! hapa ndio mnapotaka mfike!!? ukifika sehemu ukiwa juu nchini kwako tunachotegemea ni wewe kupasua mawimbi uende mbali zaidi nje ya mipaka!! lakini ukiamua kurelax hapo ulipo inamana unasubiri kushuka sababu kiukweli huwezi kukaa juu milele!!! kwanini mmeridhika hivi!!! kaka JB tatizo ni nini!!!??

Mi nakuangalia wewe kama mfano wa msanii mkubwa sana kwenye tasnia kwa sasa... mbona umerelax!!!??? umeridhika na ustar wa tanzania!!!? una kila kitu cha kukufikisha mbali... kinachohitajika ni juhudi binafsi tu ili kesho na sisi tufike mahala pazuri!! hebu tuongee wapenzi.. mnahisi huku kwenye bongo movie TATIZO LIKO WAPIII…!!???

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo kiinglish kinawapiga chenga wengi, hivyo wanaogopa kujichanganya. Mtu ambaye angeweza pia kufanya vizuri kimataifa ni Wema kwa sababu kwenye lugha yuko vzr, ila amejisahau sana labda nyie ambao mko karibu naye mumkumbushe kwamba anaweza kuibadilisha hii tasnia kwa sbbu ana jina kubwa na anaweza kuungana na waigizaji wengine wa nje ya nchi na kufanya kitu kizuri hivyo kuipaisha sanaa hii hapa Tanzania. Mwingine ni Monalisa na mama yake, Richard (sijui ameacha kuigiza), Lulu, mzee Chilo

    ReplyDelete
  2. Wameridhika na maisha ya kibongo, hapo ndo mwisho wa reli

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad