Adris wa Big Brother Abakisha Mil 200 , Atahadharishwa Asipokuwa Makini zitaisha Bila Kujua

Stori: Gladness Mallya/Ijumaa Wikienda
Mambo ya fedha! Takribani wiki saba tangu anyakue zaidi ya Sh. Milioni 500 baada ya kuibuka mshindi kwenye Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan anadaiwa kubakiza takribani kiasi cha Sh. milioni 200 baada ya kudaiwa kununua mjengo wa ghorofa wenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 300.
Kwa mujibu wa Idris, nyumba hiyo ipo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar hivyo kwa sasa naye ni baba mwenye nyumba.

Jamaa huyo alitarajia kuhamia kwenye mjengo huo jana Jumapili.
Mjengo huo una vyumba kadhaa, sebule mbili, bustani na eneo la kutosha la maegesho ya magari.
Habari zinadai kwamba kama kweli ametumia kiasi hicho cha fedha huku akimshukuru mtu aliyemtaja kwa jina la Mohamed kwa kufanikisha jambo hilo, basi atakuwa amebakizi milioni 200 ambazo wataalam wa mambo ya uchumi wanamshauri kufungulia kampuni au biashara.

Wataalam hao walifafanua kwamba, Idris anatakiwa kuzitumia fedha hizo kujiongezea kipato la sivyo atazitumia kuhudumia nyumba hiyo kwa vitu kama kulipia bili mbalimbali, kodi na kuajiri wahudumu.
“Anaweza akaona kwamba kununua nyumba ni matumizi mazuri ya fedha alizoshinda lakini anatakiwa awe makini, aidha kwa kufanyia biashara au kutoa huduma itakayokuwa ikimwingiza kipato.

“Pia asisikilize watu wanasema nini juu ya fedha zake. Anatakiwa kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo kabla hajazipata,” alisema mmoja wa wataalam hao ambaye hakupenda jina lake liandikwe.
GPL
------------------------------
Some days are just bad days, that's all. You have to experience sadness to know happiness, and I remind myself that not every day is going to be a good day, that's just the way it is!

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NI VIZURI AIPANGISHE KWANI ITALIPA

    ReplyDelete
  2. Hiyo nyumba itakuwa asset nzuri kama ataipangisha kwa wenye uwezo wa kumlipa kodi ya kueleweka then hela hiyo aitumie kuongeza kipato then na yeye ajenge au anunue nyumba simple ya kuishi halafu the balance afanyie biashara itakayomlipa! Kwa sasa afocus kuzalisha pesa zaidi asitake mambo ya kuishi kisuper star then baadae maisha mazuri yatakuja tu

    ReplyDelete
  3. HAPO UMETUMIA AKILI NYUMBA UNAPANGOSHA TENA KWA DOLLARI UNAKULA KODI KWA TARATIBU HONGERA SAANA. MWENZIO YULE RASTA SIJUI HATA KAMA ANA KITU JAPO YEYE ALIPATA DOLLAR 100,000.

    ReplyDelete
  4. Acheni uongo kaongea clouds hiyo nyumba kapewa hajatumia hata mia yake.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad