Askofu aonya wagombea kuwatoa wenzao kafara 2015

Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, limeoyesha wasiwasi wake kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kuibuka kwa matukio ya kishirikina  kwa ajili ya kupata uongozi.

Askofu msaidizi wa jimbo hilo, Eusebius Nzigilwa, alisema kitendo hicho ni cha kipagani na kamwe Watanzania wanapaswa kuwaepuka kama ukoma wagombea wa namna hiyo na wale watakatumia fedha kama ushawishi wa kuwachagua.


Askofu Nzigilwa alitoa kauli hiyo jana wakati akihubiri katika sherehe ya upadrisho wa  Padri Tito Rwegoshora na  mafrateli watatu kupewa daraja la ushemasi.

Alisema ni jukumu la Watanzania kuliombea taifa liepukane na roho ya kipagani kwa wagombea dhidi ya  Watanzania wengine wakati wa mchakato wa uchaguzi Mkuu.

“Mwaka huu tunaingia katika uchaguzi mkuu, wa kumchagua  rais, wabunge na madiwani, hivyo Watanzania tunapaswa kuwa makini n kwa kuliombea Taifa,” alisema.

“Sitabiri vifo, jitokezeni kwenda kugombea, ila msiende huko kufanya upinzani  wa ‘makafara’ wagombea wenzenu kama Herode alivyowaua wazaliwa wa kwanza wa kiume,” alisema.

Alisisitiza kuwa viongozi watoa rushwa na wale wanaoangamiza wagombea wenzao wasichaguliwe kwa kuwa maangamizi na rushwa vinakiuka maadili ya uangozi bora.

Aidha, Askofu Nzigilwa  alisema kuwa Herode alishukuru kuzawili kwa Yesu Kristo kisiasa, moyoni mwake alihofia kuzaliwa kwa mfalme wa wayahudi kungeleta mapinduzi katika uongozi wake.

“Roho ya Herode ya kuua watu tunaziona hadi leo, sisi tunaomtafuta Yesu sasa tujiulize tunakwenda kwa Yesu kumsujudia au kumwangamiza,” alisema.
Aliwaonya waliopata upadirisho na ushemasi kutotumikia mabwana wawili, anasa na Mungu, bali wanapaswa kutumikia wito wao wa kichungaji.


CHANZO: NIPASHE
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Halafu hawa Maaskofu Wanga,Mimi kanisa nimemalizana nalo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad