Askofu Gwajima mtetea Lowassa 'Bila fedha huwezi kuwaza suala la Urais'

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa mara ya kwanza amejitosa kwenye harakati za Urais kwa kutoa kauli za ukosoaji zinazowalenga baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoutaka Urais.

Katika mazungumzo yake na RAI, Gwajima alisema kauli zilizotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Januari Makamba na Waziri Mkuu wa zamani Cleopa Msuya dhidi ya wanasiasa wenzao zina dhamira ovu ya kupakana matope.

Akizungumzia kauli hizo, Askofu Gwajima alisema wanasiasa wanaodai kuchukizwa na mafisadi na kusema kwamba Watanzania wasiwachague wagombea urais wanaotumia fedha, hawana hoja badala yake wanaendesha vita ya Urais.

"Kwani mtu yeyote mwenye akili timamu anajua kwamba bila fedha huwezi kujenga mtandao wa Urais, ili ufanikiwe unahitaji kutumia fedha kujenga mtandao, kwa mfano unahitaji usaidizi wa watu wa Rukwa, Mwanza n.k; lazima uwe na watu huko Rukwa na Mwanza na lazima utoe fedha ili watu hao waweze kusafiri, kula na kulala."

"Bila fedha huwezi kuwaza suala la Urais, maneno yao yanalenga kupotosha watu kwamba wako watu fulani wasiotumia fedha, huku wakijua ukweli kwamba kila mtu anatumia fedha, kwa mfano fomu ya kuwania Urais ni shilingi milioni tano, sasa wao hizo fedha watakuwa wamezipata wapi? Kiujumla, hatua kubwa kama ya Urais inahitaji fedha," alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad