Aunty Ezekiel Afunguka na Kusema Mume Wake Hajui Kama Ana Mimba

Aunty Ezekiel Ndani ya Club
Stori:Musa mateja
Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amefunguka kuwa, licha ya ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa yoyote juu ya kitumbo hicho.Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Aunt alisema maneno hayo yanaweza kuwashangaza watu lakini ndiyo ukweli wenyewe.

Alidai kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana na hajapewa talaka kama watu wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama mtarajiwa na hata akijua hawezi kumuacha.

“Kiukweli mume wangu hajui kuwa nina ujauzito na hata akijua wala hawezi kuniacha, ananipenda sana. Sijaachana naye na wala sijapewa talaka, hayo yanayosemwa ni umbeya tu,” alidai Aunt.  
Credits:Global Publishers

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dunia imekwisha, yani anatamba kabisaaaa kwamba anamme lakini jamaa mwingine kamdunga mimba, dah!!!! cyo mchezo!!!

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu usishangae ndiyo mambo ya kuiga haya, na ndiyo mambo yanayofanya wazungu wengi wasiwe na ndoa na ndiko tunakoenda suala la kuoa litakua si la muhimu sana sababu maadili yameharibika wanawake wanataka kuonja kila mboga na wanaume nao wanataka kuonja kila mboga.

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu usishangae ndiyo mambo ya kuiga haya, na ndiyo mambo yanayofanya wazungu wengi wasiwe na ndoa na ndiko tunakoenda suala la kuoa litakua si la muhimu sana sababu maadili yameharibika wanawake wanataka kuonja kila mboga na wanaume nao wanataka kuonja kila mboga.

    ReplyDelete
  4. Wanaume miaka nenda miaka walikuwa/wamekuwa wakizaa nje ya ndoa na kuwapelekea wake zao hao watoto, upepo umegeuka sasa wanawake wanafanya wazi wazi.

    Wako wanawake kwenye ndoa waliokuwa wakiwabambikia waume zao watoto ambao si wao miaka nenda miaka rudi, ila huyu Auntie kaweka wazi tu hakutaka kuwa mnafiki angalau mumewe atajua na kufanya maamuzi anayotaka. Hebu chunguza watoto ulio nao kwako wote ni wa kwako? Una uhakika 100%?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad